Home Habari za michezo FT: TZ PRISONS 0-1 SIMBA SC….MKUDE AWAFANYIA ‘UNUNGUNUNGU’ ASKARI MAGEREZA…ONYANGO AKIRI KUOMBA...

FT: TZ PRISONS 0-1 SIMBA SC….MKUDE AWAFANYIA ‘UNUNGUNUNGU’ ASKARI MAGEREZA…ONYANGO AKIRI KUOMBA KUSEPA …


JONAS Mkude, kiungo wa kazi ndani ya Simba amepachika bao pekee la ushindi mbele ya Tanzania Prisons dakika ya 85 na kuipa pointi tatu muhimu.

Ulikuwa ni mchezo huru kwa timu zote mbili ndani ya dakika 90 kwa kila timu kutengeneza mashambulizi ya kushtukiza katika kusaka ushindi.

Dakika 45 zilikuwa ngumu kwa timu zote mbili kupata bao ambapo umakini wa kipa wa Prisons, Benedict Haule uliwafanya washambuliaji wa Simba wakiongozwa na Moses Phiri kukwama kufunga.

Uimara wa Aishi Manula uliwazuia washambuliaji wa Prisons wakiongozwa na Samson Mbangula walikwama kumtungua Air Manula.

Shukran kwa Shomari Kapombe aliyepiga faulo iliyoingia ndani ya 18 na kukutana na kichwa cha Kibu Dennis aliyempa pasi Mkude.

Mikono ya Abel wa Prisons inapaswa pongezi kwa kuwa ilikuwa imara kwenye kuokoa hatari za nyota wa Simba.

Simba inafikisha pointi 10 baada ya kucheza mechi nne, unakuwa mchezo wa kwanza kwa Juma Mgunda, kukaa kwenye benchi la mchezo huo.

Katika hatua nyingine, Mlinzi wa Simba, Joash Onyango amekiri kuwa alituma maombi ya kutaka kuondoka kwenye timu hiyo mara baada ya kushindwa kupata nafasi wakati wa Zoran Maki.

Hata hivyo, Onyango amesema kuwa sasa ameamua kujikita kuitumikia timu hiyo, huku akiomba mashabiki kutoa sapoti ya kutosha.

SOMA NA HII  KAMA HALI ITAENDELEA HIVI SIMBA HAINA NAMNA NI KIPIGO TU