Home Geita Gold FC GEITA GOLD WAKUTANA NA YA YANGA KWA SAIDO NTIBANZONKIZA…TFF WAONDOA JINA LAKE...

GEITA GOLD WAKUTANA NA YA YANGA KWA SAIDO NTIBANZONKIZA…TFF WAONDOA JINA LAKE KWENYE MAJINA YA CAF….


Nyota wa Geita, Mrundi Saido Ntibazonkiza ambaye amesaini mkataba na timu hiyo akitokea Yanga jina lake halijaonekana kwenye wachezaji wa timu hiyo wanaoiwakirisha kimataifa.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa orodha ya wachezaji 40 ambao watashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika huku jina la Saido halimo katika orodha hiyo.

Akizungumza suala hilo Katibu wa timu hiyo Simon Shija amesema:

“Mpaka sasa sijajua nini kinaendelea kwa kuwa nilikuwa kwenye kikao kuanzia asubuhi” amesema Shija na kuongeza

“Lakini tulifuata utaratibu wote wa CAF hivyo sifahamu nini kimetokea, tunachosuburi ni barua rasmi itakayotupa maelekezo na hapo ndipo tutaweza kulizungumzia hili,”

Mchezaji huyo ambae ameonyesha uwezo wake kwenye mchezo wa kirafiki baada ya kutoa pasi za mabao katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Pamba.

SOMA NA HII  BENCHIKA KUENDELEZA REKODI LEO MBELE YA ASEC MIMOSAS?....KRAMO AWAPA TAHADHARI...