Klabu ya Young Africans ya jijini Dar Es Salaam, leo imesaini mkataba mpya wa udhamini na kampuni ya GSM wenye thamani ya jumla ya Tsh Bilioni 10.9 kwa miaka mitano.
Mkataba huo uliogawanyika sehemu mbili utahusisha, mkataba wa kwanza wa uzalishaji na usambazaji wa jezi pamoja na bidhaa mbalimbali za klabu ambapo kila mwaka GSM group itailipa Yanga SC Tsh Bilioni 1.5 ambayo itakua inaongezeka kwa 10% na kufanya jumla ya thamani kuwa Tsh Bilioni 9.15 ndani ya miaka mitano.
Mkataba wa pili utakua ni wa udhamini ambapo GSM italipa Tsh Milioni 300 kwa mwaka itakayokuwa ikiongezeka kwa 10% kila mwaka kwa muda wa miaka 5 kuifanya jumla kuwa na Tsh Bilioni 1.83 kwa miaka mitano
Akizungumzia makubaliano hayo mbele ya waandishi wa habari, Rais wa klabu ya Young Africans EngHersi Said alisema
“Tunayo furaha kubwa kuingia makubaliano haya mapya na wenzetu wa GSM, moja ya ajenda zangu katika uongozi wangu ilikuwa ni kuipa klabu uimara wa kiuchumi ili tuweze kujitegemea. Na mikataba kama hii inaiongezea klabu thamani na kuiimarisha kimapato, na kama tujuavyo uendeshaji wa vilabu vyetu kunahitaji uiamara wa kiuchumi”
“Niwapongeze kampuni ya GSM kwa kuendelea kuwekeza katika klabu yetu uwekezaji wa namna hii sio tu kunaongeza thamani timu yetu bali inasaidia kwa namna nyingine kukuza soka nchini kwetu kwa ujumla”
“Niwaombe na Wanachama wa Young Africans SC waendelee kuiunga mkono kampuni ya GSM kwa kunununa bidhaa na huduma zao ili waendelee kunufaika na udhamini wao kwetu”
Kwa upande wa mdhamini, Mkurugenzi wa Biashara toka GSM Group Bw. Allan Chonjo alisema. “GSM imeona matunda makubwa sana.