Home Habari za michezo HILI HAPA KINDA LA YANGA LINALOWATOA UDENDA WAFARANSA…MARSEILLE WATUMA MTU KUMBEBA…ZAHERA ATEMA...

HILI HAPA KINDA LA YANGA LINALOWATOA UDENDA WAFARANSA…MARSEILLE WATUMA MTU KUMBEBA…ZAHERA ATEMA ‘UBUYU’…


Klabu ya Yanga imepokea mualiko wa mshambuliaji wake kinda, Clement Mzize ambaye anatakiwa na klabu kubwa ya Olympic Marseille ya Ufaransa.

Mkurugenzi wa ufundi wa Yanga Mwinyi Zahera amesema tayari Marseille wameshatuma mualiko wa kinda huyo kutakiwa kwa majaribio ya wiki mbili yatakayofanyika nchini humo.

Marseille ambao wamemuona kinda huyo katika Mashindano ya soka la vijana chini ya miaka 20 ambapo mshambuliaji huyo alionyesha kiwango bora akifunga mabao 7 na kuwa mfungaji Bora.

Tayari Yanga imeshapokea mualiko wa Clement ambaye anasubiri kupata visa tayari kwa safari ya nchini Ufaransa katika majaribio hayo.

Yanga imemjumuisha kinda huyo katika kikosi chao cha msimu huu ambapo katika mechi tatu ambazo Yanga ilicheza za kirafiki kabla ya ligi kuanza alipachika mabao mawili wakati Yanga ikiichapa Friends Rangers kwa mabao 9-0.

“Huo mualiko upo klabuni viongozi wanaufanyia kazi nafikiri katika majaribio hayo atafanikiwa kwa kuwa nimekuwa naye naona ubora wake kwa umri wake Marseille hawataweza kumuacha,”amesema Zahera.

“Ni mtoto hodari sana ana nguvu na anajua kufunga naona jinsi Tanzania inapata shida katika kuwa na wafungaji wazuri,huyu Clement kama atatunzwa vizuri na kuendelezwa na yeye mwenyewe kujitambua atakuja kuwa mtu Bora katika taifa hili.

SOMA NA HII  WAKATI MAWAZO YA SIMBA YAKIWA KWA WASAUZI KWANZA...YANGA WAIBUKA NA KUTOA MSIMAMO WAO...