Home Habari za michezo ISHU YA KUWA KOCHA MKUU KABISA…AHMED ALLY ‘AMSILIBIA DOLE GUMBA MGUNDA’ …ADAI...

ISHU YA KUWA KOCHA MKUU KABISA…AHMED ALLY ‘AMSILIBIA DOLE GUMBA MGUNDA’ …ADAI TIMU ILIKUWA HAIPAMBANI…


Msemaji wa Simba SC, Ahmed Ally amesema Kocha Mkuu wao wa muda Juma Mgunda anatosha kuifundisha klabu hiyo licha ya kuwa mchakato wa kumtafuta kocha wa kudumu unaendelea.

Ahmed amesema, Kocha huyo ana hadhi ya kuifundisha Simba kwa sababu anayo leseni A na alipoingia, ameonesha kitu cha tofauti.

“Anatosha, ni kocha mwenye viwango kwa maana amesom kuanzia hatua ya kwanza hadi hatua hiyo ya juu. Mgunda tangu amefika ameonesha kitu cha tofauti. Timu inapambana, Ile hali ya kupambana ndio ilikosekana Simba kwa mechi zile za awali licha ya kuwa tulishinda,” alisema Ahmed.

SOMA NA HII  JEMEDARI SAID: INAKERA...YANGA WAKISHINDA WAMENUNUA MECHI... ILA SIMBA NI SAWA..?