Home Habari za michezo JEMEDARI SAID: TFF INAWEZEKANA INAONEAGA…..LAKINI KWA HILI YANGA MMEJIONEA WENYEWE….!

JEMEDARI SAID: TFF INAWEZEKANA INAONEAGA…..LAKINI KWA HILI YANGA MMEJIONEA WENYEWE….!


Kufuatia sakata la mchezaji wa Congo DR, Tuisila Kisinda kuzuiliwa kusajiliwa na Yanga akitokea RS Berkane ya Morocco, mchambuzi wa soka nchini, Jemedari Said amesema Yanga wamelikoroga wenyewe.

Tangu jana kumekuwa na lawama kedekede mitandaoni zikielekezwa TFF kwamba wana agenda binafsi na mabingwa wa nchi Yanga SC kwa kitendo chao cha kuzuia usajili wa Kisinda.

Wenye nasaba na Yanga na walio karibu na Viongozi wamejaribu kuichafua TFF kwa kusema INAIONEA Yanga.

Nimejaribu kufatilia jambo hili na nikagundua kwamba Yanga INAJIONEA yenyewe na wapambe wanataka tu kuipaka matope TFF kwa kutotaka kusema ukweli.

Ukweli ni kwamba Yanga SC, Simba SC, Azam FC na Geita Gold FC zote zilishafanya na kumaliza mapema usajili wao wa wachezaji wa Kimataifa na kupewa Leseni zao.

Walifanya mapema kwakuwa usajili wa CAF lazima uwe na Leseni ya ndani kama kiambatanishi ili upate leseni ya CAF kwajili ya Inter clubs competition zao.

Ili kuendana na muda wa usajili CAF, TFF ikafanya UPENDELEO kwa vilabu vyake vipate leseni za ndani mapema na haraka ili wakamilishe usajili wa Kimataifa (CAF).

Yanga SC waliwakilisha majina ya wachezaji wao 12 na wakapewa na leseni za ndani kwajili ya kuambatanisha CAF. Katika hao wachezaji 12 Tuisila Kisinda jina lake halikuwepo.

Baadae Yanga wakaleta jina la Kisinda wakati wameshakamilisha usajili wa wachezaji 12 wa kigeni kama kanuni inavyotaka. Sasa TFF hawawezi kukubali usajili wake kwakuwa atakuwa mchezaji wa 13, lakini hoja pia ya kumtoa yoyote kati ya waliosajiliwa haiwezi kufanya kazi kwenye dirisha hilihili la usajili mpaka labda dirisha dogo.

Kwenye system ya usajili unaweza kuweka wachezaji wa kigeni hata 40, system inapokea kama vigezo vimekamilika. Lakini inawachukua TFF kuwaidhinisha kwa hiyo hoja ya jina la Kisinda kuingia kwenye system kabla ya dirisha kufungwa pia haina mashiko na hoja mfu.

Viongozi wakubali kwamba waliharakisha kupeleka yale majina yale ya mwanzo huku dili la Kisinda likiendelea, labda hawakuwa na uhakika litakuja kukamilika au wamegundua madhaifu wakati washamaliza wachezaji 12 wa kigeni, lakini sio kwamba kuna uonevu popote.

SOMA NA HII  BAADA YA MORRIOSN NA KAMBOLE...HAWA HAPA MASTAA WENGINE WAWILI WANATUA YANGA AISEE...NI SAPRAIZI...

BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless)