Home Habari za michezo KAMA ULIKUWA HUJUI…YANGA NA NABI WADAIWA DENI HILI LA CAF…LAZIMA LILIPWE LEO…LA...

KAMA ULIKUWA HUJUI…YANGA NA NABI WADAIWA DENI HILI LA CAF…LAZIMA LILIPWE LEO…LA SIVYO SIMBA ITAENDELEA KUWA JUU…


Kikosi cha Mabingwa wa Tanzania, Timu ya Yanga inashuka leo dimbani kutupa karata yake ya kwanza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga watakuwa ugenini majira ya saa kumi jioni kuwakabili Zalan FC kutoka Sudan katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar baada ya Zalan kuomba mchezo huo upigwe Dar kutokana na sababu za kiusalama.

Sasa wakati Yanga wakijiandaa na mchezo huo wa hatua ya awali, wanaingia wakiwa na madeni mawili makubwa.

Kwanza Yanga inaingia ikichochewa na deni la miaka 24 la kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo wamekuwa wakihaha kufika tangu walipofanya hivyo mwaka 1998.

Lakini deni la pili ambalo wanalo ni kocha Nasreddine Nabi kupata ushindi katika mechi ya kwanza ya kimataifa ya kimashindano ambapo tangu alipoanza kuinoa timu hiyo mwaka jana, hajawahi kufanya hivyo.

SOMA NA HII  SAA CHACHE KABLA YA KUKIPIGA NA MAMELOD...NABI AMNG'ATA SIKIO GAMONDI....ALICHOMWAMBIA HIKI HAPA...