Home Habari za michezo KAMA UNAUNDUGU NA MCHEZAJI WA YANGA…’CHAP HARAKA KAOMBE MSAADA’…WAMELIPWA PESA ZAO KIMYA...

KAMA UNAUNDUGU NA MCHEZAJI WA YANGA…’CHAP HARAKA KAOMBE MSAADA’…WAMELIPWA PESA ZAO KIMYA KIMYA AISEE…


Mastaa wa Yanga mambo yao yamenyooka baada ya kujazwa mkwanja kimyakimya na uongozi wa klabu hiyo kabla ya mechi ya juzi usiku.

Taarifa za uhakika zinatibitisha kwamba mkwanja huo ambao uliingizwa kwenye akaunti zao Jumatatu jioni ni posho za kumaliza ligi msimu uliopita bila kupoteza mchezo ‘unbeaten’

Kiporo hicho kiliibua mzuka kwa wachezaji hao tangu jioni hiyo. Hilo lilijiri saa kadhaa baada ya Yanga kutangaza udhamini mpya wa Sh 10.9 bilioni kutoka kwa kampuni ya GSM juzi hiyohiyo mchana.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo kililiambia Mwanaspoti, wamemalizana na mastaa wao kwenye ishu ya bonasi za ‘Unbeaten’ na mastaa wote wameahidi kupambana kibabe zaidi msimu huu kuhakikisha wanatetea mataji yote ikiwemo kufika hatua ya makundi ya Afrika.

“Ni kweli wachezaji walikuwa wanatudai lakini tumemalizana nao lengo ni kuhakikisha timu inakuwa kwenye hali nzuri za ushindani ili kuendeleza rekodi yetu ya msimu uliomalizika kwa kurudisha mataji yetu,” kilithibitisha chanzo chetu cha kuaminika ingawa uongozi uligoma kutoa tamko rasmi kwa madai ni ishu za ndani.

SOMA NA HII  KAMWE:- WAARABU TUMEWASOMA...TUMEWAPIGIA MAHESABU MAKALI...WATASHANGAA MPIRA BOLIBO