Home Habari za michezo KISA SAKATA LA CHETI CHA MGUNDA….MANARA AENDELEA KUIPIGIA KELELE TFF…AIBUKA NA SWALI...

KISA SAKATA LA CHETI CHA MGUNDA….MANARA AENDELEA KUIPIGIA KELELE TFF…AIBUKA NA SWALI HILI GUMU KWAO…


Aliyekuwa Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amesema ameshangazwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Kujibu kila kitu kinachozuka kwenye mitandao ya kijamii akisema wanakurupuka

Kauli hiyo ya Manara inakuja ikiwa ni muda mfupi baada ya TFF kutoa orodha ya makocha wenye leseni ya daraja A la CAF baada ya mijadala kuibuka kuwa kocha mkuu wa muda wa Simba Sc, Juma Mgunda hana cheti hicho hivyo hatoweza kukaa kwenye benchi kuiongoza Simba dhidi ya Nyasa Big Bullets leo.

Katika orodha ya makocha wenye leseni A iliyotolewa na TFF jana, jina la Juma Mgunda limejumuishwa ili kuondoa utata na sintofahamu iliyokuwa ikijadiliwa mitandaoni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika; “Kuna mengine mm najiandikia tu kufurahisha Baraza, sasa kila kitu mtakuwa mnajibu tu. Matokeo yake hadi Marehemu Silvester Marsh mmemuoredhesha kwa haraka ya kujibu.

“Maisha ya Instagram ni kuchetuana akili tu, nakumbuka msimu uliopita ilitokea Issue very controversial Mitandaoni kuhusu Yanga, Hersi akaniambia itabidi tutolee ufafanuzi, nikamwambia tutalikuza bila sababu, dawa ni kulipotezea litajifia lenyewe.

“Sasa hao Makocha walioambiwa wana hizo leseni wengine wanasema hawajapewa vyeti vyao, JM kapataje? Au ndio yale yale? Taasisi haipaswi kujibu kila mjadala wa mitandaoni, chukueni elimu hyo, mkijibu mtatupa nafasi ya kuhoji mengine.

“Swali, kakipataje wakati wengine hawajapewa? Sawa kasoma Cheti kapewa lini na kwa nini yeye apewe Usiku Usiku?” amesema Manara.

Baada ya kauli hiyo, TFF wameliondoa jina la Marehemu Silvester Marsh na kuacha majina 20 kwenye orodha hiyo kisha kuposti tena kupitia ukurasa wao wa Instagram.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUBURUZA MKIA ....HIVI NDIVYO SIMBA ITAKAVYOTUSUA CAF KIBABE...