Home Habari za michezo KISA VIPIGO MFULULIZO ….MSTAA IHEFU WAWEKWA KIKAANGONI…KATWILA APIGWA BUMBUWAZI ASIJUE LA KUFANYA…

KISA VIPIGO MFULULIZO ….MSTAA IHEFU WAWEKWA KIKAANGONI…KATWILA APIGWA BUMBUWAZI ASIJUE LA KUFANYA…


Kipigo cha mechi tatu mfululizo kwa Ihefu kimewafanya wachezaji, benchi la ufundi na viongozi kukaa chini ili kuwekana sawa kwa nia ya kutafuta tiba mapema kabla mambo hayawatibulia zaidi.

Ihefu iliyorejea Ligi Kuu Bara msimu huu, ilianza kwa kufungwa bao 1-0 na Ruvu Shooting, kisha ikalala tena 1-0 kwa Namungo kabla ya kufumuliwa 3-1 na Mtibwa Sugar, licha ya kikosi chao kuundwa na mastaa wengi wapya waliowahi kuwika klabu kubwa ndani na nje ya nchi.

Kocha Mkuu wa Ihefu, Zubery Katwila alisema amekaa kikao kizito na wachezaji na kuwaambia huu ni mwanzo, hivyo wasife moyo na matokeo kwani wana uwezo wa kubadilisha hali iliyopo kwa sasa kutokana na ubora walionao, lakini akitaka wabadilike na kupambana kuipa timu matokeo mazuri.

“Tumekaa chini wote na kutafakari kwa kina kipi kinatuangusha ilihali tuna timu nzuri, nashukuru tulifanikiwa kwani kila mmoja wao alieleza kile ambacho anakiona, kikubwa walichogusia na mimi nimekiona ni kupunguza makosa binafsi,” alisema nyota huyo wa zamani wa Mtibwa na Taifa Stars.

Katibu Mkuu wa kikosi hicho, Zagalo Chalamila alisema wao sio wa kwanza duniani kupitia hali iliyopo kwa sasa kwani anaamini watakapoanza kupata ushindi hapo ndipo itakuwa ni mwanzo mzuri kwao wa kuamsha morali ya wachezaji.

Baada ya vipigo hivyo, Ihefu inakabiliwa na kibarua kingine kigumu Septemba 17 itakapomenyana na KMC katika Uwanja wa Uhuru, huku timu hiyo kabla kupanda msimu huu zimekutana mara mbili ikifungwa moja kwa bao 1-0 mechi iliyopigwa Julai 18, 2021 kabla ya kulipa kisasi kwa ushindi wa bao 1-0 pia mchezo uklichezwa Desemba 19, 2020.

Ihefu ikashuka msimu huo na msimu uliopita ilipambana Ligi ya Championship hadi kurudi Ligi Kuu Bara msimu huu.

SOMA NA HII  MANARA KAONA HAITOSHI...AWAVAA WACHEZAJI YANGA KUHUSU POSHO....ADAI PATACHIMBIKA...