Home Habari za michezo KUELEKEA KLABU BINGWA AFRIKA KWA WANAWAKE…SIMBA QUEENS WAANZA KULA TIZI LA KIBINGWA…MAMBO...

KUELEKEA KLABU BINGWA AFRIKA KWA WANAWAKE…SIMBA QUEENS WAANZA KULA TIZI LA KIBINGWA…MAMBO NI πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯…


Mabingwa michuano ya Klabu Bingwa ya Wanawake kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati, Simba Queens baada ya mapumziko ya muda mfupi, Jumatatu ijayo wataingia kambini kuanza kujifua kwa ajili ya fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika itakayofanyika kuanzia Oktoba 30 nchini Morocco.

Meneja wa timu hiyo, iliyopangwa Kundi A, Seleman Makanya amethibitisha hilo, akiweka bayana mpango wa kuongeza beki wa kati na mshambuliaji mmoja kikosini kama muda utaruhusu.

β€œTupo mapumziko kidogo lakini kikosi kitaingia kambini Jumatatu kuanza maandalizi ya Ligi ya Mabingwa sambamba na ligi ya ndani.

Wachezaji wote watakuwepo na kama muda utaturuhusu tuna mpango wa kuongeza beki wa kati na mshambuliaji mmoja ili kuongeza nguvu kikosini,” alisema Makanya.

Naye kocha mkuu wa kikosi hicho, Sebastian Nkoma ameweka wazi mipango yake katika kambi hiyo kuwa ni kuwaanda wachezaji wote kuwa fiti kwaajili ya mashindano makubwa.

β€œTunaenda kuendelea tulipoishia, lengo ni kufanya vizuri kwenye kila mashindano tunayoshiriki hivyo lazima tufanye maandalizi imara,” alisema Nkoma.

Simba ndiyo itauwakilisha ukanda wa CECAFA ikiwa ni kwa mara ya kwanza kufuzu fainali hizo baada ya msimu uliopita kukwama na ukanda huu kuwakilishwa na Vihiga Queens ya Kenya.

Katika kundi la msimu huu wa michuano hiyo ya Afrika, Simba imepangwa na washindi namba tatu wa msimu uliopita, ASFAR ya Morocco, Green Buffaloes ya Zambia na Determine Girls ya Liberia.

SOMA NA HII  BILIONI 10 ZATAKIWA TIMU ZA TAIFA...RAIS SAMIA ACHANGIA MILIONI 500...