Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA CAF KESHO KUTWA…HATMA YA KAPOMBE NA MKUDE MIKONONI MWA...

KUELEKEA MECHI YA CAF KESHO KUTWA…HATMA YA KAPOMBE NA MKUDE MIKONONI MWA MGUNDA….


Shomari Kapombe na Jonas Mkude wameungana na kikosi katika safari ya kwenda kuvaana na Wamalawi, Nyasa Big Bullet.

Shomari na Mkude hawakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichocheza jana Septemba 7, 2022 dhidi ya KMC na Wekundu hao wa Msimbazi kutoka sare ya goli 2-2.

Kapombe, Mkude sambamba na Peter Banda wameonekana mapema hii kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere sambamba na nyota wengine wa timu hiyo, tayari kwa mechi hiyo ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa Septemba 10, 2022.

Simba wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa na Kocha Mkuu mpya Juma Mgunda waliyemtangaza kufanya naye kazi kwa muda baada ya kuachana na aliyekuwa kocha wao mkuu Zoran Maki.

SOMA NA HII  NJOMBE MJI YAPIGWA TAFU KIMTINDO NA BOSI