Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YAO NA SIMBA…TZ PRISONS WALAMBA SHAVU LA MKATABA MNONO WA...

KUELEKEA MECHI YAO NA SIMBA…TZ PRISONS WALAMBA SHAVU LA MKATABA MNONO WA MAMILIONI YA PESA…


Klabu ya Tanzania Prisons imeingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni ya kimataifa ya Silent Ocean ambao unalenga kuijenga zaidi klabu hiyo.

Mkataba huo utaisaidia Prisons katika chakula na usafiri, pia una kipengele cha kuongeza muda endapo makubaliano ya kimkataba yatafanikiwa kwa pande zote mbili.

Prisons inapata mkataba huo ikiwa imesalia siku moja kabla ya kuwakaribisha Simba nyumbani katika Uwanja wa Sokoine Mbeya mechi itakayochezwa Jumatano Septemba 14, 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Septemba 12, Mwenyekiti wa Tanzania Prisons, Enock Mwanguku amesema udhamini huo utakwenda kuongeza nguvu katika mambo muhimu ndani ya timu ili kufanya vizuri zaidi ya msimu uliopita ambapo walifanikiwa kubaki kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kucheza hatua ya mtoano (playoff).

Mwanguku amesema Silent Ocean imeweka zaid ya Sh50 milioni ambayo inakwenda kununua mahitaji muhimu kama vyakula, maji lakini pia kugharamia malazi na vitu vingine vya msingi ndani ya timu ili iweze kufiki malengo ya kufanya vizuri na kumaliza katika nafasi nne za juu.

Amesema ili kufanya vizuri katika michezo ya ligi unahitaji kuwa na nguvu katika masuala ya kiuchumi na ndiyo kitu walichofanya Silent Ocen na litakwenda kuwapa faida katika masuala ya kiufundi.

“Niwashukuru viongozi wa juu katika kampuni hii niwahidi tutaishi katika misingi tuliyokubaliana ndani ya mkataba na watapata kile ambacho wanahitaji kutoka kwetu na timu itaenda kufanya vizuri msimu huu tukianza na mchezo wa kesho dhidi ya Simba.” alisema Mwanguku.

Kwa upande wake Mkuu wa idara wa mauzo na masoko wa Silent Ocean, Mohammed Kamilagwa amesema wameamua kuwekeza kwa wajela jela hao baada ya kuona malengo yao waliyo nayo ya kufanya vizuri kwenye ligi msimu huu kumaliza nafasi ya nne tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita.

“Lengo lingine ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuendeleza michezo ambayo imekuwa sekta inayotoa ajira nyingi kwa kwa vijana wengi kama wale wanaopatikana ndani ya Tanzania Prisons.” amesema Kamilagwa.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUFUZU AFCON MWAKANI...KILICHOIBEBA TAIFA STARS MBELE WA WAARABU HIKI HAPA...