Home Habari za michezo KWA MPANGO HUU WA YANGA….MECHI IJAYO ‘LITAKUFA JITU’ AISEE…NABI AMVUTA ‘CHOBINGO’ AZIZ...

KWA MPANGO HUU WA YANGA….MECHI IJAYO ‘LITAKUFA JITU’ AISEE…NABI AMVUTA ‘CHOBINGO’ AZIZ KI…


Katika kuhakikisha wanapambana na mabeki jeuri na wababe uwanjani, Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi, amebadili gia na kuwapa mastaa wake, Fiston Mayele na Stephane Aziz Ki program mbili tofauti za fitinesi.

Hiyo ikiwa ni siku chache mara baada ya kuona wachezaji wake wanachezewa rafu za makusudi kutokana na kupaniwa na wapinzani tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Yanga ndani ya michezo mitatu ya mashindano kwa kuanzia Ngao ya Jamii na Ligi Kuu Bara, imewakosa wachezaji wawili kutokana na majeraha waliyoyapata akiwemo Salum Aboubakari ‘Sure Boy’ na Jesus Moloko.

Jumamosi iliyopita, Nabi aliwapa program ya mazoezi ya fitinesi kwenye Ufukwe wa Coco, Masaki jijini Dar es Salaam.

Nabi akiongozana na kocha wake msaidizi, Cedric Kaze na wa viungo, Helmy Gueldich raia wa Tunisa, ndiye alikuwa akisimamia program hizo za mazoezi.

Program hiyo ilianza saa 12:00 asubuhi na kumalizika saa 2:00 asubuhi akitumia takribani dakika 120 kuwapa mazoezi ya fitinesi kwenye uwanja unaotumiwa mashindano ya Beach Soka.

Helmy aliwataka wachezaji hao kukimbia mbio fupi na ndefu ndani ya wakati tofauti sambamba na kuruka koni ambazo zilipangwa katika uwanja huo.

Kocha huyo wa viungo jana Jumatatu saa 2:00 asubuhi aliendelea na program ya fitinesi kwenye Viwanja vya Gymkhana, Posta jijini Dar es Salaam wakitumia saa mbili pekee.

Timu hiyo inafanya maandalizi hayo kujiandaa na mchezo wa Dar es Salaam Dabi dhidi ya Azam FC utakaopigwa Septemba 6, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Pia inajiandaa na mchezo wake wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika watakaocheza dhidi ya Zalan FC ya Sudan Kusini.

SOMA NA HII  WAKATI BARBARA AKIWAKILISHA SIMBA KWENYE MKUTANO WA CAF...YANGA WAIBUKA NA HOJA HIZI BAADA YA KUTOPEWA MWALIKO....