Home Burudani KWA NGUVU YA 1000…KATOKA KUWA MUUZA DUKA MPAKA KUWA MILIONEA WA PERFECT...

KWA NGUVU YA 1000…KATOKA KUWA MUUZA DUKA MPAKA KUWA MILIONEA WA PERFECT 12 JACKPOT YA M-BET….

 


Kuna usemi wa vijana kwamba maisha hayana formula.Hii imejidhihirisha kwa kijana Raphael ambaye ameibuka mshindi wa milioni 113.7 kutoka M-Bet na kumfanya kuingia kwenye orodha ya madigala ‘milionea’ hapa nchini.

 Anasema ushindi wake umekuja baada ya kuamua kutokata tamaa kwani  kabashiri  zaidi ya mara 100 kwenye kwenye Perfect 12 jackpot.

Siku ya Jumatatu 29, Agosti 2022 itabaki kuwa historia kwa kijana huyu ambaye ni kibarua katika moja ya duka la vinywaji lililopo Ubungo Dar es Salaam.

 “Mchezo wa Crystal Palace dhidi ya Brentford FC  ulikuwa mgumu sana kwangu kutabiri kutokana na matokeo ya awali, nilishindwa kubashiri haraka na baada ya kufikiria sana, nilibashiri matokeo ya sare na ndivyo ilivyokuwa,” alisema Daudi.


Raphael anaeleza kuwa moja ya ndoto kubwa maishani mwake ni kufungua biashara yake ili aweze kutengeneza kipato kikubwa zaidi.

Tokea kuanza kwa mwaka huu Daudi ni mshindi wa nane wa mwaka huu kuibuka mshindi katika jackpot ya PERFECT 12  Allen Mushi, Mkurugenzi Masoko wa M-Bet Tanzania alisema.

 Mushi pia aliwaomba Watanzania wenye umri zaidi ya miaka 18 kuendelea kubashiri kupitia M-BET ili waweze kubadili maisha na kushinda mamilioni ya fedha.

 Stephen Adili, Mkuu wa Kitengo Cha Wateja Binafsi wa Benki CRDB alimpongeza Daudi kwa kushinda kiasi kikubwa cha fedha na kumshauri kutumia kiasi hicho cha fedha kuwekeza.

 “Nampongeza Daudi kwa ushindi huu mkubwa na kikubwa zaidi ni mteja wa benki yetu yenye ushirikiano mkubwa na kampuni ya M-Bet Tanzania.

 PERFECT 12 ni Jackpot inayotolewa na kampuni ya kubashiri ya M-Bet Tanzania ambapo mteja anatakiwa kubashiri kwa shilingi 1000, mechi 12 kwa usahihi ili aweze kujishindia dongo nono.

 

SOMA NA HII  KISA KOCHA MPYA KUTOKA HISPANIA..RAGE AUNYOOSHEA KIDOLE UONGOZI WA SIMBA..AITAJA YANGA...