Home Habari za michezo MZIMU WA MOSIMANE WAENDELEA KUISUMBUA AL AHLY…WAINGIA GHARAMA KUBWA KUMPA KAZI “M’BAYA...

MZIMU WA MOSIMANE WAENDELEA KUISUMBUA AL AHLY…WAINGIA GHARAMA KUBWA KUMPA KAZI “M’BAYA WA CHELSEA”…


Klabu ya Al Ahly imemtangaza Marcel Koller raia wa Uswizi kuwa kocha wake mkuu baada ya kuingia naye mkataba wa miaka miwili na atawasili klabuni hapo leo Jumamosi akiwa na wasaidizi wake watatu kuanza kazi.

Kocha aliyewapa mafanikio Ahly, Pitso Mosimane raia wa Afrika Kusini aliachana na Ahly baada ya kufungwa bao na Wydad Casablanca mwezi Mei, katika mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Mabingwa Afrika.

Mreno Ricardo Soares alichukua nafasi hiyo lakini ameshindwa kuonyesha kile ambacho Mafarao hao wa Misri walikitarajia kutoka lwake baada ya kushindwa kutwaa ubingwa wa Misri na kumaliza nafasi ya tatu, ambayo hawajawahi kuishika tangu msimu wa mwaka 1991/92 hovyo Soares akatimuliwa ikiwa ni miezi miwili tu tangu ajiunge nao.

Koller (62) ambaye ameanza kazi ya ukocha mwaka 1997, amewahi kufundisha vilabu vya:-

1997–1998 FC Wil

1999–2002 St. Gallen

2002–2003 Grasshoppers

2003–2004 FC Köln

2005–2009 VfL Bochum

2011–2017 Austria (Timu ya Taifa)

2018–2020 FC Basel

Koller amepata mafanikio akiwa na Gallen mwaka mmoja tu baada ya kujiunga nao akichukua Kombe la Ligi ya Uswizi kwa mara ya kwanza tangu walipochukua mara ya mwisho miaka 100 nyuma na kufanikiwa kuifunga Chelsea katika michuano ya UEFA Cup. Pia, alitwaa tuzo ya kocha bora wa mwaka wa Uswizi mnamo mwaka 2000.

Koller ndiye aliyeibua kipaji cha mchezaji Lukas Podolski akiwa FC Köln nchini Ujerumani.

Amewahi kuifundisha timu ya Taifa ya Australia na katika kipindi chake ndipo timu hiyo ilifanikiwa kufuzu fainali za Euro kwa mara ya kwanza ikishika nafasi ya 10 katika timu bora duniani kwa mujibu wa FIFA.

Akiwa FC Basel, Koller ameisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi ya Uswizi kwa misimu miwili mfululizo. Ametinga nusu fainali ya Europa kabla ya kupigwa na Eintracht Frankfurt bao 4-0 kwa aggregate na kuondoshwa katika hatua hiyo.

Kwa ujumla, Koller ana mataji manne akiwa kama kocha, yakiwemo mataji mawili ya ligi kuu ya Uswizi na moja la Bundesliga 2 na moja la Swiss Cup.

SOMA NA HII  KIRAKA HUYU KUTOKA SIMBA KUTUA KAGERA SUGAR