Home Habari za michezo NABI ALIA NA KOSA KOSA ZA KINA MAYELE YANGA….AMBUNDO ANYOOSHEWA KIDOLE….NKANE AANZA...

NABI ALIA NA KOSA KOSA ZA KINA MAYELE YANGA….AMBUNDO ANYOOSHEWA KIDOLE….NKANE AANZA KUINGIA INGIA…


KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema ana kazi kubwa ya kuimarisha safu yake ya ushambuliaji hasa katika michezo ya kimataifa katika hatua zinazofuata za michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, CAF.

Kauli hiyo aliitoa juzi, Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam baada ya kupata ushindi wa mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Zalan FC katika mchezo wa awali wa michuano hiyo huku kipindi cha kwanza wakishindwa kuzitumia nafasi nyingi walizotengeneza.

Yanga inatarajia kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya Zalan FC Jumamosi wiki hii na mshindi wa jumla atatinga raundi ya kwanza kukutana na ama St. George ya Ethiopia au Al Hilal ya Sudan.

Nabi alisema mechi haikuwa rahisi kipindi cha kwanza kwa sababu walicheza na timu hawaifahamu ubora na madhaifu yao, hivyo kupata wakati mgumu wa kufumania nyavu dakika 45 za kwanza.

Alisema walitengeneza nafasi nyingi za wazi, lakini washambuliaji hawakuwa makini hali iliyosababisha kutopata ushindi katika kipindi cha kwanza ila cha pili walibadili mchezo kwa kufanya mashambulizi ya pembeni.

“Ambundo (Dickson), alicheza vizuri na kukosa nafasi ya wazi pia alikosa kujiamini na tuliona madhaifu yao, hivyo tukamtoa na nafasi yake kuchukuliwa na Nkane (Denis) ambaye tulimpa jukumu la kupeleka mashambuluzi ya pembeni, kutafuta  matokeo”.

“Tumekosa mambo mengi hili ni la kufanyia kazi hasa baada ya kusonga katika hatua inazofuata, ninaamini hizi mechi mbili tutakuwa tunazitumia kwa ajili ya kuona mapungufu yetu na kufanyia kazi kwa kutengeneza muunganiko wa wachezaji,” alisema Nabi.

SOMA NA HII  HATIMAYE YANGA WAFUNGUKA...ISHU YA FEISAL SALUM "FEI TOTO"...WAMEZUNGUMZA HAYA