Home Habari za michezo PAMOJA NA KUWA MFUNGAJI MZURI YANGA…FEI TOTO AVUNJA UKIMYA KUHUSU NAMNA ANAVYOCHEZESHWA...

PAMOJA NA KUWA MFUNGAJI MZURI YANGA…FEI TOTO AVUNJA UKIMYA KUHUSU NAMNA ANAVYOCHEZESHWA NA NABI…


Nyota wa Yanga, Feisal Salum ameweka wazi kuwa ni furaha kwake kufunga kwa ajili ya kuipa matokeo timu yake jambo ambalo anaamini kwamba litaendelea

Septemba 6,2022 Feitoto alitupia mabao mawili kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC uliokamilika kwa wababe hao kutoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.

Ni Azam FC waliaza kupachika bao la kuongoza kupitia kwa Daniel Amoah na lile la pili lilifungwa na beki Ndoye.

Kiungo huyo aliingia dakika ya 45 akichukua nafasi ya Dennis Nkane aliweza kufunga mabao hayo yote mawili akiwa nje ya 18.

“Nimetimiza jukumu langu la kuipa matokeo timu nitaendelea kufunga mabao nikiwa nje ya 18 kwa kuwa hii sio mara yangu ya kwanza.

“Ambacho ninaamini ni kwamba kikubwa ni kuendelea kufanya kazi na kushirikiana na wachezaji wenzangu kwa ajili ya kufanya vizuri,” amesema Feisal.

Kiungo huyo mzawa ni namba moja kwa wenye mabao mengi ndani ya Yanga akiwa nayo mawili sawa na Fiston Mayele wa DR Congo

SOMA NA HII  YANGA WATINGA CONGO YASEPA NA BEKI, WAIBUKIA AFRIKA KUSINI