Home Habari za michezo PAMOJA NA SIMBA KUFUNGWA JUZI….MAKI KAKIANGALIA KIKOSI CHAKE WEEE..KISHA KWA UPOOLE AKASEMA...

PAMOJA NA SIMBA KUFUNGWA JUZI….MAKI KAKIANGALIA KIKOSI CHAKE WEEE..KISHA KWA UPOOLE AKASEMA HAYA…

WAKATI kikosi cha Simba kilirejea nchini jana kikitokea Sudan, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Zoran Maki, amefurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake katika mechi ya kirafiki ya kimataifa ya mwisho waliyocheza dhidi ya wenyeji, Al Hilal hapo juzi.

Maki alisema mechi hiyo imeendelea kuwapa nafasi ya kujiimarisha wachezaji wake na imewasaidia kuwaweka tayari na mapambano katika mechi za Ligi Kuu Bara na mashindano ya kimataifa.

“Ingawa tumefungwa bao 1-0, lakini tumecheza vizuri sana, tulimiliki pia, hatukutengeneza nafasi nyingi katika mechi mbili au tatu zilizopita, kwa mfano nafasi aliyocheza Banda (Peter) ya kiungo ilikuwa bora sana, ilikuwa suprise kubwa kwangu,” alisema Maki.

Naye kiungo, Clatous Chama, alisema mechi walizocheza zimewasaidia kuwaimarisha na wanashukuru hawajapata majeraha kwenye michuano hiyo maalumu waliyoshiriki.

“Kuna baadhi ya wachezaji walikosekana, lakini hii ni timu na kila mmoja alijaribu kuonyesha uwezo wake, tumepata nafasi ya kujijenga, imetupa nafasi ya kujifunza sisi na benchi la ufundi tukiwa kwenye maandalizi ya kuelekea Malawi,” Chama alisema.

Wakati huo huo, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema uongozi wa klabu hiyo umeweka wazi beki wao, Joash Onyango, hataondoka katika kikosi hicho na badala yake atatakiwa kupambana kupata namba.

“Bado ana mkataba ambao unamfunga, ataendelea kuwapo kikosini na yupo katika mipango ya benchi lao la ufundi,” Ahmed alisema.

Alisema baada ya kurejea nchini jana wataingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo mwingine wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Arta Solar 7 kutoka Djibouti ili kujiimarisha kuelekea mechi yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KMC FC itakayochezwa Septemba 7, mwaka huu.

SOMA NA HII  HIZI HAPA SABABU YA KIFO CHA MCHEZAJI WA U17 WA SINGIDA BIG STAR ALIYEFIA UWANJANI LEO..