Home Habari za michezo SAA CHACHE BAADA YA KUPEWA TIMU…MGUNDA ATOA MSIMAMO WAKE KUFANYA KAZI NA...

SAA CHACHE BAADA YA KUPEWA TIMU…MGUNDA ATOA MSIMAMO WAKE KUFANYA KAZI NA MATOLA…”MNIOMBEE SANA JAMANI”…


Saa chache baada ya Simba SC kumtangaza Kocha Juma Mgunda kuwa Kocha wa Muda, Kocha huyo mapema leo Alfajiri ameongozana na kikosi kuelekea Malawi tayari kwa mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Simba SC itacheza dhidi ya Mabingwa wa Malawi Nyassa Big Bullet Jumamosi (Septemba 11) katika Uwanja wa Bingu mjini Lilongwe.

Mgunda alitangazwa kuwa Kocha Mkuu wa Muda, huku Simba SC ikiendelea na mchakato wa kumsaka Kocha Mkuu mpya atakayechukua nafasi ya Zoran Maki aliyevunja mkataba kwa makubaliano maalum.

Akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Kocha Mgunda, alizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema hana budi kumshukuru Mungu kwa uteuzi huo, huku akiwataka Mashabiki wa Simba SC kumuombea ili afanikishe jukumu lake salama.

“Ninaomba mniombee kwa sababu nina jukumu zito sana kwa mujibu wa kazi yangu, Simba SC ni timu kubwa ninahidi kupambana kwa kushirikiana na mdogo wangu Matola.”

“Ninamuhitaji sana Matola katika kipindi hiki, kwa sababu yeye amekulia humo, ninaamini tutasaidiana vizuri kuanzia mchezo wa Kimataifa tunaokwenda kucheza Malawi.” amesema Mgunda

Juma Mgunda amejiunga na Simba SC kwa muda akitokea Coastal Union ya jijini Tanga.

SOMA NA HII  WIKIEND INAKUJIA NA ODDS BOMBA KUTOKA MERIDIANBET....CHAKUFANYA KWAKO NI HILI...