Home Habari za michezo SAKATA LA KUROGWA NA POGBA….MBAPPE AVUNJA UKMYA..AANIKA A-Z KUHUSU ANAYOYAJUA…MGANGA ALIHUSIKA SANA…

SAKATA LA KUROGWA NA POGBA….MBAPPE AVUNJA UKMYA..AANIKA A-Z KUHUSU ANAYOYAJUA…MGANGA ALIHUSIKA SANA…


Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain (PSG) ya nchini Ufaransa Kylian Mbappe ameungana na kiungo wa Juventus, Paul Pogba katika sakata la uchawi linalomkabili Pogba.

Paul Pogba amewaambia wachunguzi kwamba watu wanaoambaza taarifa hizo, akiwemo kaka yake Mathias, walikuwa wakitaka kumchafua kwa kudai alimwomba mganga amroge Mbappe.

Mbappe sasa amevunja ukimya wake kuhusu hali hiyo na amefichua mazungumzo ambayo amekuwa nayo na mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya Ufaransa.

Mshambuliaji huyo wa PSG aliulizwa ikiwa sakata hilo limeathiri uhusiano wake na Paul Pogba na akajibu,”hapana, kwa sababu leo ​​napendelea kuamini neno la mchezaji mwenzangu, alinipigia simu na kutoa neno lake kuhusu hili tukio, na sasa ni neno lake dhidi ya kaka yake. Nitamwamini mwenzangu kwa maslahi ya taifa na timu pia.”

“Tuna mashindano makubwa (Kombe la Dunia) na tayari ana matatizo, sio wakati wa kumpa jingine, tutaona jinsi yatakavyokuwa. Nimejitenga na yote”

Kwa upande wa Pogba anadai kwamba aliomba msaada wa mganga ili kujisaidia kukomesha majeraha yanayo mkabili na sio kumroga Mbappe.

Paul Pogba amekuwa na wakati mgumu kutokana na majeraha na bado hajaonekana katika kikosi cha Juventus tangu arejee kutoka Manchester United msimu huu wa joto.

SOMA NA HII  BARCELONA KUMUUZA COUTINHO KWA DAU LA HASARA