Home Habari za michezo SAKATA LA USAJILI WA KISINDA KUKATALIWA….MANARA AZIDI ‘KUWAPELEKEA MOTO TFF’..AKUMBUSHIA ISHU YA...

SAKATA LA USAJILI WA KISINDA KUKATALIWA….MANARA AZIDI ‘KUWAPELEKEA MOTO TFF’..AKUMBUSHIA ISHU YA KAHATA NA SIMBA…


Baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutoa ufafanuzi kuhusu kuukataa usajili wa mchezaji wa Yanga, Tuisila Kisinda raia wa Congo DR kwa madai kuwa tayari majina 12 ya wachezaji wa kimataifa wa klabu hiyo yalishapitishwa na shirikisho hilo, Haji Manara ameibuka na jipya tena.

Msemaji huyo wa Yanga SC ambaye ameshafungiwa na TFF kujihusisha na masuala ya soka kwa kipindi cha miaka miwili, ameandika;

“Hata haieleweki kimejibiwa kitu gani? Na kwa nini ishu ya Yanga uharaka wa kujibu unakuwa mkubwa mno? Kanuni hizi hizi zilizombadilisha Chikwende kwa Kahata? Kanuni hizi hizi zilizomhalalisha Kibu kucheza bila kupata uraia?

“Au mnazungumzia zipi ndugu zangu? Kazi yenu na kusaidia wachezaji wacheze mpira na sio kuwazuia na ndio maana bila baraka zenu ITC ya Kisinda isingepatikana na faini alilipishwa nani?

“Last season tena kwa maksudi, Yanga pamoja na kuomba kucheza na washabiki kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa, hamkupeleka barua CAF. Matokeo yake Club ikakosa mapato mengi kwenye mchezo dhidi ya Rivers ya Nigeria, na sio mapato tu, kucheza bila mashabiki nyumbani kunaweza kuchangiwa na kutolewa mapema kwenye Mashindano yale.”

“Wiki hiyo hiyo wenzetu Team Pendwa walicheza na Washabiki wao. TFF kanuni kuwa favoured ni kwao tu ila Kwa Yanga zinavunjwa? Mbona hamkuwahi kujibu kuhusu kuwanyang’anya Yanga haki ya kucheza bila mashabiki? Naendelea kuwakumbusha, yana mwisho haya,” amesema Manara.

SOMA NA HII  KISA KUITWA MZEE....RONALDO ASHINDWA KUMVUMILIA ROONEY...AMCHANA HADHARANI...