Home Geita Gold FC SIKU KADHAA BAADA YA KUTANGAZWA KUSAJILIWA GEITA…NTIBAZONKIZA AIBUKA NA KUANIKA UKWELI WOTE….

SIKU KADHAA BAADA YA KUTANGAZWA KUSAJILIWA GEITA…NTIBAZONKIZA AIBUKA NA KUANIKA UKWELI WOTE….


Amerudi tena na ameanzia alipoishia hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya mshambuliaji Said Ntibazonkiza ‘Saido’ kurudi tena katika ardhi ya Tanzania kwa mara ya pili baada ya kuamalizana na waajili wake wa zamani Yanga.

Saido raia wa Burundi msimu huu amerudi kuitumikia Geita Gold ambayo inashiirki mashindano ya kimataifa ikiwashiriki nchi kwa mara ya kwanza katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Geita imepata nafasi hiyo baada ya kumaliza nafasi ya nne Ligi Kuu msimu ulioisha. Tayari Saido ameshaonyesha mchango wake kwenye mechi ya kirafiki kwa kutoa pasi mbili za mabao 2-0 dhidi ya Pamba.

Mrundi huyo amerudi akiwa ameacha rekodi yake tamu ndani ya Yanga akiitumikia timu hiyo kwa misimu miwili na kuondoka nchini Mei 29, 2022 baada ya kumaliza mkataba wake.

Saido pamoja na kuondoka na kuwaaga wachezaji wenzake hakuwa na furaha kwani aliibuka kwenye tukio baya akiwa na Dickson Job baada ya kutoroka kambini wakati timu hiyo ikijiandaa na mchezo wa nusu fainali ya ASFC dhidi ya Simba.

Makala hii inakuchambulia baadhi ya alama alizoziacha Yanga ndani ya misimu miwili aliyokaa tangu ajiunge nayo msimu wa 2020-2022 dirisha dogo la usajili.

9 Ndio mabao aliyofunga ndani ya misimu miwili alipokuwa akiitumikia Yanga akianza na mabao mawili kwenye msimu wake wa kwanza baada ya kucheza dakika 280. Alifunga mabao mawili dhidi ya Dodoma Jiji dakika ya 68, Yanga ikishinda mabao 3-1, mchezo uliopigwa Arusha, Desemba 19, 2020 bao lingine alifunga dhidi ya Tanzania Prisons katika sare ya 1-1 dakika ya 77 Desemba 31, 2020.

Katika msimu wake wa pili aliingia kambani mara saba alianza kwa kuisawazishia timu yake kwa bao la penalti dhidi ya Namungu FC dakika 80, mchezo uliopigwa Novemba 23, Uwanja wa Majaliwa (1-1).

Mengine ni dhidi ya Mtibwa Sugar dakika 50 Februari 23 (Manungu) Yanga ikishinda mabao 2-0, Mbeya Kwanza dakika ya 17 shuti la mbali (Sokoine, Novemba 30) timu yake ikishinda mabao 2-0.

Mbeya Kwanza dakika 38 (Mkapa, Mei 20),Yanga mabao 4-0, penalti na Biashara United dakika ya 79 (Mkapa, Desemba 26) Yanga mabao 2-1, Coastal Union dakika ya 80, (Mkwakwani, Januari 16 )Yanga 2-0 na Kagera Sugar dakika 64 (Mkapa, Februari 27), Yanga 3-0.

8 Ni asisti alizotoa kwenye misimu miwili aliyocheza Yanga. Katika msimu wa kwanza alitoa nne na msimu wa pili nne. Alianza kwa kutoa pasi zilizozaa mabao kwenye mechi tatu dhidi ya Dodoma Jiji dakika ya 75 alitoa asisti ya bao lililofungwa na Bakari Mwamnyeto, Yanga ilishinda mabao 3-1.

SOMA NA HII  UGOMVI WA NABI NA SAIDO WAFIKIA HATUA HII YANGA...APEWA ADHABU MBELE YA WACHEZAJI WENZAKE

Ushindi wa mabao 3-0 ulioipata Yanga alihusika na mabao mawili akitoa pasi ya bao dakika ya 12 kwa Deus Kaseke, dakika ya 50 kwa Yacouba ya bao la pili, nyingine ilikuwa dhidi ya KMC dakika ya 46 bao la Yacouba, mchezo huo ulipigwa Aprili 10, 2021 Benjamin Mkapa, mchezo ulimalizika kwa bao 1-1, dakika ya 43 kwa Khalid Aucho (Benjamin Mkapa, Desemba 19, 2021).

Dhidi ya Prisons alitoa asisti ya bao la Khalid Aucho dakika 43, ( (Nelson Mandela Desemba 19, 2021), Yanga 2-1, Kagera Sugar asisti ya bao la Fiston Mayele dakika ya 30 na 51(Mkapa, Februari 27), assisti nyingine ni dhidi ya Tanzania Prisons bao la Khalid Aucho Desemba 19, 2021.

Kocha Fredy Felix ‘Minziro’ anasema anatambua ubora na umuhimu wa mchezaji huyo ndani ya kikosi chake anatarajia kuona akiibeba timu yake kutokana na uzoefu alionao kwenye mashindano ya ndani na nje.

“Haikuwa rahisi kumpata ndani ya timu yetu umetumika ushawishi mkubwa hadi kutua Geita Gold tunatarajia makubwa kutoka kwake ni mchezaji mzuri na mzoefu atasaidia timu yetu kwenye ligi na mashindano ya kimataifa,” anasema na kuongeza;

“Ujuo wake utaongeza nguvu hasa eneo la ushjambuliaji ni mtu ambaye anajicho zuri kwenye kutoa pasi za mwisho kazi kwao washambuliaji wangu hasa George Mpole ambaye ameshakuwa mzoefu kwenye timu pia kuna mshambuliaji mzuri wa kigeni.”

SAIDO ANENA

Saido anasema kazi yake kubwa ni kuchea mpira na kurudi kwake nchini ni katika kuhakikisha anaendelea kukitumikia kipaji chake.

“Kazi yangu ni mpira nimerudi Tanzania kwasababu nimehitajiwa tena baada ya kutambua uwezo wangu, hivyo sasa ni mwajiriwa wa Geita Gold nimekuja kucheza nategemea ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wachezaji wenzangu kazi iliyonileta nitaifanya kama inavyotakiwa,” anasema na kuongeza;

“Sina ugeni kwenye Ligi ya Tanzania nitafanya kile nitakachoweza kufanya kuhakikisha naisaidia timu yangu kupata matokeo. Pia, nafahamu kuna kazi nyingine ya kufanya kimataifa tutapambana kuhakikisha tunafanya vizuri ili kuweza kufikia malengo.”