Home Habari za michezo SIMBA WAFUNGUKA JINSI MAREHEM DK GEMBE ALIVYOCHANGIA MAFANIKO YAO …MASTAA WAKUBWA WAMUAGA..

SIMBA WAFUNGUKA JINSI MAREHEM DK GEMBE ALIVYOCHANGIA MAFANIKO YAO …MASTAA WAKUBWA WAMUAGA..


PATRICK Rweyemamu, Meneja wa Simba ameweka wazi kuwa mafanikio ya timu hiyo huwezi kuyataja na kumuweka pembeni Dk Yassin Gembe.

Gembe alitangulia mbele za haki Septemba 2,2022 ambapo taarifa ilitolewa na uongozi wa Simba ilieleza Gembe aliyekuwa daktari wa timu ya wanaume (Senior Team) kilitokea kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Leo Septemba 4, imefanyika ibada ya kumuaga Gembe ambapo wachezaji na familia ya michezo imeweza kufika Mbweni kwa ajili ya kuhani msiba.

Rweyemamu amesema: “Sisi tuliobahatika kuishi na kufanya kazi na Dkt. Gembe tumepoteza mtu wa kipekee.

” Mafanikio ya Simba yaliyopatikana sasa hauwezi kumweka pembeni sababu alikuwa na mchango wake kuandaa timu kwenda kwenye mchezo,” .

Miongoni mwa wachezaji wa Simba ambao walikuwa kwenye kuaga mwili wa Gembe ni pamoja na Erasto Nyoni,Ally Salim,Sadio Kanoute.

Pumzika kwa amani.

SOMA NA HII  KISA SIMBA NA YANGA... KLABU YA STRAIKA LA MABAO KUTOKA KUTOKA UGANDA YAIBUKA NA HILI JIPYA...WATAKA ML 348.6..