Home Habari za michezo SIMBA WAIFANYIA UMAFIA NYASA BIG BULLETS …CHAMA AWAVURUGA WAMALAWI…WAPAGAWA NCHI NZIMA…

SIMBA WAIFANYIA UMAFIA NYASA BIG BULLETS …CHAMA AWAVURUGA WAMALAWI…WAPAGAWA NCHI NZIMA…


Wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC wameanza vyema kampeni ya kusaka kufuzu kwa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi ugenini nchini Malawi.

Simba wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi, magoli yaliyowekwa wavuni na Mshambuliaji Moses Phiri kipindi cha kwanza na John Bocco mwishoni mwa kipindi cha pili.

Gumzo kubwa katika mchezo wa Simba leo ni ufundi wa Kiungo wake raia wa Zambia Clatous Chotta Chama ambae ameonesha kandanda safi lililowapoteza Wamalawi.

Ushindi wa Simba ni hatua nzuri kwa Kocha mpya ndani ya Kikosi hicho Juma Mgunda ambae anasiamama kama kocha Mkuu katika kikosi hicho.

Simba watarudiana na Nyasa Big Bullets katika mchezo wa mkondo wa Pili utakaopigwa Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

SOMA NA HII  MAMBO NI MOTO CHAMPIONSHIP KOCHA MWINGINE ATUPIWA VIRAGO