Home Geita Gold FC WAKATI SIMBA NA YANGA WAKIWA NA UHAKIKA CAF…GEITA GOLD WAAPA KUWEKA...

WAKATI SIMBA NA YANGA WAKIWA NA UHAKIKA CAF…GEITA GOLD WAAPA KUWEKA REKODI YAO KIMATAIFA LEO…


Kocha Msaidizi wa Geita Gold, Mathius Wandiba amesema hawatarajii kurudia makosa waliyoyafanya mechi iliyopita wanahitaji ushindi ili waweze kusonga hatua inayofuata.

Geita Gold wanatarajia kuwa wenyeji wa Hilal Alhasil ya Sudan leo  mchezo unaotarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao 1-0 ugenini.

Akizungumza na waandishi wa habari, Wandiba alisema wamefanyia kazi makosa waliyoyafanya mechi iliyopita wanatarajia mchezo mzuri na wa ushindani kutokana na ubora wa wapinzani wao.

“Wapinzani wetu ni wazuri na sisi ni bora pia tunatarajia ushindani mkubwa lani malengo yetu kama klabu ni kupata matokeo kwenye uwanja wetu wa nyumbani,” alisema.

Akizungumzia suala la kinara wa mabao, George Mpole ambaye alikosekana mechi iliyopita alisema anaendelea vizuri na amefanya mazoezi ya mwisho na timu suala la kucheza au kuto kucheza wao kama benchi la ufundi wataamua.

“Geita Gold kukosa matokeo kwenye mechi ya kwanza haina uhusiano wowote na kukosekana kwa Mpole kwani timu ina kikosi kipana lakini kurejea kwake itategemea na namna tutakavyopanga kikosi anaweza akachesa au asicheze.”

Alisema wachezaji wao wote wapo kwenye hali nzuri ya mchezo hawatarajii kumkosa mchezaji yoyote kutokana na ugonjwa au

SOMA NA HII  KIBU AWAINGIZA VITANI SIMBA NA YANGA...MRITHI WA LOMALISA YUPO NJIA PANDA