Home Geita Gold FC WAKATI WAKISHINDA WANAKUTANA WA WAMISRI…MPOLE KUWAPA NGUVU GEITA GOLD LEO…WAKIZEMBEA NDIO BASI...

WAKATI WAKISHINDA WANAKUTANA WA WAMISRI…MPOLE KUWAPA NGUVU GEITA GOLD LEO…WAKIZEMBEA NDIO BASI TENA…


MSHAMBULIAJI wa Geita Gold, George Mpole ameanza rasmi mazoezi na kikosi hicho kwa ajili ya mchezo wa marudiano hatua ya awali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Hilal Alsahil ya Sudan, mchezo utakaopigwa leo katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Nyota huyo alikosa mechi ya kwanza iliyopigwa Sudan Septemba 11 kutokana na kusumbuliwa na Malaria huku akishuhudia kikosi hicho kikifungwa bao 1-0.

Mpole alisema kwa sasa afya yake imeimarika tofauti na wiki moja iliyopita hivyo ni suala tu la benchi la ufundi kumtumia katika mchezo huo muhimu huku akiwa na shauku kubwa ya kuona timu yake inasonga mbele.

“Niwatoe hofu mashabiki zangu kwani nimeanza mazoezi na nipo tayari kuipambania timu yangu, siku zote kukosea ndio njia sahihi ya kujifunza hivyo kupoteza mechi ya kwanza kwetu haijatuvunja moyo kwani imetuongezea motisha,” alisema Mpole na kuongeza;

“Watu wanazungumza mengi kuhusu mimi hususani la kutokufunga msimu huu ila wanashindwa kuelewa hata msimu uliopita nilikaa michezo mitano pasipo kufunga, hivyo naamini ni mwanzo na nafasi ya kutetea kiatu changu nilichochukua bado iko wazi.”

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Fred Felix ‘Minziro’ alisema kurejea kwa nyota huyo kunawapa matumaini makubwa ya kupindua matokeo ya mechi ya kwanza huku akisisitiza nidhamu zaidi kwa wachezaji wake ili kufuzu kwa hatua inayofuata.

Mshindi wa jumla baina ya timu hizo atacheza na Pyramids ya Misri katika raundi ya pili itakayoanza kuchezwa kati ya Oktoba 7, 9 kwa mechi za kwanza huku marudiano ni Oktoba 14 hadi 16.

SOMA NA HII  HII CAF SUPER LEAGUE NI SUPA KWELI KWELI AISEE...BINGWA KUKOMBA ZAIDI YA BILIONI 200..WAKATI TIMU SHIRIKI ZIKIPEWA BIL 6...