Home Habari za michezo WASUDAN WAPARAMIA ‘MTUMBWI WA VIBWENGO’ KWA MKAPA…MAYELE ‘AWAPAPATUA TATU NA TUMBO’ JUU…

WASUDAN WAPARAMIA ‘MTUMBWI WA VIBWENGO’ KWA MKAPA…MAYELE ‘AWAPAPATUA TATU NA TUMBO’ JUU…


Kikosi cha Zalan FC wamekubali kichapo cha magoli 4-0 kutoka kwa wawakilishi wa Tanzania Yanga, mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar.

Mchezo huo wa hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika umewashuhudia Yanga wakitawala sehemu kubwa ya mchezo.

Alikuwa ni Fiston Mayele aliewapa uongozi Yanga sekunde chache tangu kuanza kwa kipindi cha pili kabla ya Feisal Salum kupachika bao la pili 55′ akimaliza kazi safi ya Fiston Mayele.

Dakika za 85 na 87 Mayele alirudi tena kambani na kupachika mabao 2 na kuhitimisha Hat-trick.

Yanga watarudiana na Zalan wikiendi ijayo mchezo wa mkondo wa pili kumpata mshindi wa jumla atakaekwenda hatua inayofuata.

SOMA NA HII  YANGA WANAPOMKATAA KISINDA LEO HUKU WAKITAKA MUJIZA YA USAJILI...