Home Habari za michezo YANGA YA INJII HERSI NI BALAA SANA….HIVI NDIVYO WALIVYOKAMLISHA USAJILI WA KISINDA...

YANGA YA INJII HERSI NI BALAA SANA….HIVI NDIVYO WALIVYOKAMLISHA USAJILI WA KISINDA KIJASUSI…SIMBA WALIMTAKA…


TUISILA Kisinda amerejea kwa mara nyingine ndani ya kikosi cha Yanga akitokea Klabu ya RS Berkane.

Nyota huyo raia wa DR Congo anasifika kwa soka la spidi na kuwa mmoja ya viungo ambao wana kasi kubwa wawapo uwanjani.

Anakumbukwa namna alivyokuwa akiwapa tabu wapinzani wake alipokuwa ndani ya Yanga ikiwa ni pamoja na kumsababisha penalti kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba iliyokamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said ameonekana akiongea naye na kumwambia kwamba karibu kwa mara nyingine Yanga.

Kisinda ameweka wazi kuwa anarejea kufanya kazi na yeye anajua majukumu yake huku mtu wake wa karibu akitonya kuwa Simba nao walikuwa wanamtaka mara baada ya kufeli kwa dili la Manzoki.

Unakuwa ni usajili wa kufungia kazi kwa Yanga ambayo imewasajili pia Gael Bigirimana, Bernard Morrison na Aziz KI.

SOMA NA HII  BENCHIKHA AMPA ONYO HILI JEAN BALEKE