Unaambiwaje, Wikiendi hii boli litatembea kwenye viwanja tofauti barani ulaya, ni Ligi ya Epl, La Liga, Serie A, Ligue 1 na Bundesliga pamoja na ligi nyingine za mataifa ya Ulaya. Kamata ratiba ya mechi zenye Odds kubwa kutoka Meridianbet.
Ni raundi ya 14 ya epl kuwakutanisha Mabingwa watetezi Man City watakaokuwa ugenini dhidi ya Leicester City, Haaland anakismati cha kufunga magoli. Hii ngoma itapigwa mapema tu siku ya Jumamosi, Bashiri kupitia Meridianbet
Chelsea ya Graham Potter itakuwa ugenini dhidi ya Brighton kutafuta alama 3 muhimu, huku Brighton wakiwa wanazihitaji alama 3 ili wajiweke sehemu salama zaidi kwenye msimamo wakiwa nafasi ya 9 mpaka sasa. Liverpool nao watakuwa Anfield kukipiga dhidi ya Leeds United. Mechi hizi zimepewa Odds kubwa na machaguo mengi zaidi.
Arsenal wakiwa wanaongoza Ligi mpaka sasa kwenye dimba la Emirates, unadhani wataendeleza ubabe wao walioanza nao msimu huu dhidi ya Nottingham Forest ambao walimnyoa Liverpool wiki iliyopita. Pale Old Trafford boli litatembea wakati United watakapokutana na West Ham, ni Antony na Ronaldo kuwazamisha West Ham? Meridianbet pekee ndiyo mabingwa na sehemu sahihi ya kubashiri.
Kwenye La Liga utawashuhudia Barcelona ya Xavi watakipiga dhidi ya Valencia huku Sevilla akiwakaribisha Royal Vallecano na siku ya Jumapili Real Madrid watakuwa nyumbani dhidi ya Girona, wakati huo Real Sociedad watakiwasha na Betis.