Home Habari za Yanga ACHANA NA KIPIGO CHA WASUDAN JANA…ALLY KAMWE APATA PIGO LINGINE….MASTAA YANGA WAUNGANA...

ACHANA NA KIPIGO CHA WASUDAN JANA…ALLY KAMWE APATA PIGO LINGINE….MASTAA YANGA WAUNGANA NAYE…

Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe

Msemaji wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mwanaye, Latiffah Ally Kamwe wakati akiwa Addis Ababa, Ethiopia kuelekea Khartoum nchini Sudan kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Al Hilal.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kamwe ameandika; “Ndani ya uwanja wa Bole, pale Addis Ababa, Ethiopia. Dakika chache kabla hatujaunga ndege kwenda Khartoum, nilipokea meseji ya kuumiza sana kwenye simu yangu.

“Ali, mtoto amefariki”. Binti yangu mdogo, Latiffah alikuwa ameaga dunia.

Nilishituka sana. Mikono ikatetemeka. Mwili ukapata ganzi ya ajabu.

Sikuamini. Ni kama mshale ulirushwa ghafla kwenye mgongo wangu. Nikaanza kusikia maumivu makali moyoni.

Nikajipa ujasiri wa kupiga simu ya Mama yake.. Alipokea, Lakini hakuweza kutoa neno lolote zaidi ya kilio kilichosindikizwa na kwikwi kali.

Nikapoteza ujasiri. Sikio langu lilishindwa kuendelea kumsikia Mama Latiffah akiendelea kulia. Nikakata simu na hapa ndio nikaamini kuwa Latiffah hayupo tena duniani.

Ukiwa mzazi, utanielewa pindi unapopata Taarifa ya kifo cha ghafla cha mtoto ambaye uliondoka nyumbani na kumuacha salama kabisa.

Allah, mpangaji wa kila jambo alipanga pumzi chache kwenye kifua cha mwanangu. Alhamdulillah ????

Nashukuru kwa viongozi wa @yangasc kuanzia Rais @caamil_88, CEO @andremtine kaka zangu @simon.esq @cpa.mfikirwa @walterharson kwa kunifariji

Shukrani pia kwa wachezaji wa @yangasc ???? Haikuwa rahisi kwangu hata kidogo kuishi Sudan huku ukijua kuna sehemu ya maisha yako haipo tena..

Lakini niliuvisha moyo wangu koti la ujasiri. Kila nilipohisi kushindwa, nilikimbia chumbani na kujifungia.. Nikitoa nje naendelea na kazi.

Sikutaka wengine waone ni jinsi gani nimesambaratika moyoni.. ALHAMDULILLAH ????

Rest in Peace Tiffah..☁️ Baba Atakuona tena wakati mwingine” ????

SOMA NA HII  KISA MANARA KUOMBA MSAMAHA KWA WAZIRI....JEMEDARI SAIDI AIBUKA NA KUMPA TENA 'MAKAVU LIVE'...

1 COMMENT