Home Habari za michezo AHMED ALLY : MECHI DHIDI YA SIMBA, YANGA WAICHUKULIA KAMA WORLD CUP...

AHMED ALLY : MECHI DHIDI YA SIMBA, YANGA WAICHUKULIA KAMA WORLD CUP YAO….

Habari za Simba

Msemaji wa Klabu ya Simba SC, Ahmed Ally amesema katika mchezo wa Jumapili, Oktoba 23, 2022, timu yao haitaruhusu wapinzai wao wa Jadi, Yanga kuondoka na ushindi kwani wamejidhatiti kuondoka na pointi tatu muhimu.

“Pamoja na ukubwa tulionao Afrika lakini ni lazima tutawale soka la ndani. Lazima vilabu vya ndani vituogope kama wanavyotuogopa wengine huko nje. Hapo ndo inakuja umuhimu wa kushinda mchezo wa Jumapili ili kulinda heshima yetu.

“Haina maana kama unawafunga watu huko Afrika lakini humu ndani kuna timu inakusumbua. Ingawa tunajua wenzetu hii ndo World Cup yao, wachezaji wao waliwasajili kwa ajili ya mechi hii, viongozi wao mafanikio yao yanapimwa na mechi hii lakini jukumu letu kama Simba ni kutoruhusu watimize malengo yao kupitia sisi.

“Hatutataacha kitu Jumapili, hatupo tayari kuwapa faraja watu waliovunjika mioyo. Tunataka kuendeleza tabasamu kwa mashabiki wetu na tunataka kukaa kileleni tukiwa comfortable,” amesema Ahmed Ally.

SOMA NA HII  ALLY MAYAY: SIMBA NA YANGA ZINATEGEMEANA KATIKA MAFANIKIO