Home Habari za michezo ALLY KAMWE: YANGA KUKOSA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA NI UKWELI UNAOUMA…

ALLY KAMWE: YANGA KUKOSA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA NI UKWELI UNAOUMA…

Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa kwa klabu kubwa kama Young Africans kukaa miaka 24 bila kucheza hatua ya makundi, ukisimuliwa unaweza ukaona kama utani.

Ally Kamwe ameyasema hayo kupitia Wasafi FM, jana Ijumaa, Oktoba 21, 2022 wakati Yanga ikijiandaa na mchezo wa derby dhidi ya Simba SC siku ya Jumapili.

”Ukweli mchungu lazima sisi tukabiliane nao, kwa klabu kubwa kama Yanga miaka 24 bila kucheza hatua ya makundi, ukisimuliwa unaweza ukaona kama utani, miaka 24 Yanga hajacheza makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, shauku ya mashabiki ni kubwa mno kuona timu inafanikiwa kwenye hilo.

”Mkishindwa kutofanikisha hilo hamtakiwi kujibizana na mashabiki kwa sababu wao matarajio yao, shauku yao ni kuona timu inavunja huo mwiko, imeshindikana wametoa maoni yao na klabu imeyasikia na wachezaji wameyasikia,” amesema Ally Kamwe.

Yanga ambao malengo yao yalikuwa ni kuingia hatua ya makundi ya ligi ya Mabingwa Afrika lakini Al Hilal FC wakazima ndoto za Wananchi hao kwa kuwatoa sasa wapo Kombe la Shirikisho ambako huko wamepangiwa na Club Africain ya Tunisia mchezo wa kwanza ukitarajiwa kupigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Novemba 2, 2022.

SOMA NA HII  MWAKINYO: WAZANZIBAR HAWATUTAKI...HUU MUUNGANO UNAUNGANISHA NINI..?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here