Home Habari za Simba KUELEKEA KARIAKOO DABI….MO DEWJI AMFUNIKA VIBAYA MNOO GSM…AWEKA MEZANI MIL 500 CASH…

KUELEKEA KARIAKOO DABI….MO DEWJI AMFUNIKA VIBAYA MNOO GSM…AWEKA MEZANI MIL 500 CASH…

Kuelekea kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi, Rais wa Heshima wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’, ameahidi zaidi ya Sh 500Mil kwa wachezaji na benchi la ufundi kuhakikisha wanashinda pambano hilo ili wasivuruge furaha ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Jumapili hii, Yanga atakuwa mwenyeji katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, ambapo atawakaribisha watani wake Simba, baada ya kuwafunga kwenye mchezo wao wa mwisho wa Ngao ya Jamii kwa mabao 2-1, yaliyofungwa na Fiston Mayele huku la Simba likifungwa na Pape Sakho.

Chanzo chetu kutoka Simba kimeliambia Championi Jumatano kwamba, baada ya Simba kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya C.D. Primeiro de Agosto ya Angola, Mo aliwataka wachezaji na benchi la ufundi kuhakikisha wanaendeleza furaha hiyo kwa kuwafunga Yanga.

Kilisema kuwa ili kuhakikisha hamasa na morali ya wachezaji inaongezeka ndani ya uwanja, ameahidi kuwapatia wachezaji wake Sh 500Mil kama bonasi ili wapambane na kuhakikisha furaha na shangwe zinaendelea kubaki kwa mashabiki wao.

“Mchezo wetu wa Jumapili dhidi ya Yanga, tumeuona ni mgumu, tayari tajiri Mo Dewji ameahidi kitita ili vijana wetu watupatie ushindi kwa lengo la kuendeleza shangwe ya mashabiki.

“Mo anaamini kufungwa na Yanga kutavuruga furaha yote ya mashabiki ya kufuzu hatua ya makundi kimataifa, hivyo ni lazima tuthibitishe ubora wetu katika ligi.

“Na itakuwa aibu kwetu tufungwe kwa mara ya pili katika msimu huu, tumefungwa na Yanga katika Ngao ya Jamii, hivyo katika ligi hatutakubali tufungwe kirahisi.

“Hivyo tajiri kaahidi kutoa bonasi ya zaidi ya Sh 500Mil kama vijana wetu watashinda na hiyo ni nje kabisa ya bonasi za kawaida zinazotolewa katika kila ushindi wa mechi kubwa kama hii ya dabi,” kilisema chanzo hicho.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally na kusema kuwa:

“Ni kweli tumejipanga kuhakikisha tunashinda kwenye mchezo huo, ila kuhusu bonansi na taarifa hizo za Rais wetu wa heshima kwa sasa sijui japo ninafahamu kuwa mechi kama hizo huwa kweli kuna fungu huwa linatoka kwa wadau na hata viongozi.”

SOMA NA HII  HARUNA MOSHI 'BOBAN' vs CHAMA....NANI AANZE KIKOSI CHA SIMBA ....?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here