Home Habari za michezo PAMOJA NA KUPIGWA JUZI….YANGA WALAMBA MKATABA NA UMOJA WA MATAIFA…

PAMOJA NA KUPIGWA JUZI….YANGA WALAMBA MKATABA NA UMOJA WA MATAIFA…

Leo Oktoba 18, 2022, Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC imetia saini mkataba wa miezi sita na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto – UNICEF unaolenga kuongeza uelewa wa umma kuhusu chanjo ya UVIKO-19 na uhamasishaji kuhusu virusi vya Ebola.

Katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Yanga SC, Andre Mtine ameeleza kuwa leo siku ya kihistoria kwa klabu hiyo kuingia mkataba mkubwa na shirika kubwa duniani.

Rais wa Klabu, ENg. Hersi amezungumzia vipi mkataba huu?

Mnamo Septemba 20, 2022 serikali ya Uganda ilitangaza mlipuko wa virusi vya Ebola katika eneo la magharibi mwa nchi. Rais wa Yanga, Hersi Ally Said, alisema kuwa ni heshima kubwa kuingia mkataba na UMOJA WA MATAIFA.

Alisema ni kwa mara ya kwanza katika historia kwa vilabu vya hapa Afrika Mashariki.

Akaongeza pia ushirikiano na UNICEF umejengwa katika falsafa ya timu yake ya kusaidia jamii. “Tunajulikana kama timu ya wananchi. Falsafa yetu ni kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto zinazowakabili wananchi,” Hersi alisema.

“Tunashirikiana na UNICEF ili kila shabiki na mpenzi wa Yanga – na vilabu vingine – apate maarifa na uelewa kuhusu chanjo ya UVIKO-19. Ni jukumu letu kama klabu kuunga mkono juhudi zitakazotuwezesha kushinda UVIKO-19 na Ebola,” Hersi alisisitiza.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, Tanzania imetoa zaidi ya dozi milioni 26 za chanjo ya UVIKO-19. Idadi ya kesi zilizothibitishwa nchini ni 39,513 kufikia Oktoba 7, 2022.

Upande wa UNICEF wanasemaje?

“Yanga imetuonyesha umuhimu wa michezo kwenye kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya afya,” alisema Bi Fatimata Baladi, mwakilishi wa UNICEF Tanzania.

“Ushirikiano wetu utasaidia zaidi ya mashabiki milioni 25 wa soka nchini Tanzania kupata taarifa sahihi kuhusu chanjo ya UVIKO-19 na virusi vya Ebola ili waweze kujilinda,” Bi. Fatimata alieleza.

Aidha amesema kuwa kutokomeza magonjwa ya milipuko kama vile UVIKO-19 na Ebola kunahitaji juhudi za pamoja kutoka kwa washikadau katika nyanja mbalimbali.

Makubaliano hayo yalifikiwa wakati serikali na wadau wengine wakiwemo washirika wa maendeleo wakishirikiana kwa karibu kuzuia mlipuko wa Ebola nchini.

Kupitia ushirikiano huu na Yanga, mashabiki wa michezo na jamii kwa ujumla watajifunza njia za kujikinga na virusi hivi.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO DILI LA MAKUSU YANGA LILIPOFIKIA...FRAGA KUKABIDHIWA MIKOBA YA LWANGA SIMBA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here