Home kimataifa SADIO MANE ALIVYO’IZIKA’ BARCELONA JANA…ATUNGUA GOLI LA MAPEMA ZAIDI…

SADIO MANE ALIVYO’IZIKA’ BARCELONA JANA…ATUNGUA GOLI LA MAPEMA ZAIDI…

HALI ilikuwa mbaya kwa Barcelona kwenye mchezo wa UEFA Champions League ndani ya dakika 90 kwa kuwa hakuna shuti hata moja walilopiga likalenga lango.

Katika mashuti 9 waliyopiga ilikuwa ngumu kupenya kwenye ngome ya Bayer ya Msenegal Sadio Mane ambaye alianza kuwatungua dakika ya 10 kwenye mchezo huo.

Licha ya kuwa walikuwa Uwanja wa Camp Nou walishuhudia wakichapwa mabao 3-0 na kuwafanya wabaki na pointi zao 4 wakiwa nafasi ya tatu kwenye kundi C baada ya kucheza mechi tano.

Mabao mengine yalifungwa na Eric Maxim Choupo-Moting dakika ya 31 na lile la tatu lilijazwa kimiani na Banjamin Parard dakika 90+5 na kuwafanya wawe nafasi ya kwanza na pointi 15.

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA WAKIIKATAA GSM...MANARA AIBUKA NA YA KWAKE...ADAI WANA 'UZEZETA'...AITAJA NBC...