Home Burudani WATZ WALIOTIKISA ‘GOT TALENT’ WAFUNGUKA WALIPOANZIA…WADAI HAIKUWA RAHISI..

WATZ WALIOTIKISA ‘GOT TALENT’ WAFUNGUKA WALIPOANZIA…WADAI HAIKUWA RAHISI..

Watanzania Ibrahim Ramadhan na Fadi Ramadhan almaarufu Ramadhan Brothers, waliong’ara katika mashindano ya Australia’s Got Talent yaliyofanyika usiku wa Jumapili, Oktoba 16, 2022, wamefunguka mambo mengi kuhusu maisha yao ikiwemo jinsi walivyoanza sarakasi.

Ramadhan Brothers wamesema walianza sarakasi tangu wakiwa watoto wadogo lakini walikuwa wakicheza mitaani mpaka walipokuja kugunduliwa vipaji vyao na kocha wao ambaye ndiye aliyewaunganisha kimataifa.

Ramadhan Brothers wamepita kwa kubonyezewa Golden Buzzers ambayo huheshimika duniani kote katika michezo mbalimbali na wanapewa nafasi kubwa ya kuibuka washindi katika fainali zinazotarajiwa kumtoa mshindi mwezi ujao nchini Australia.

SOMA NA HII  MDHAMINI WA SIMBA FREDY 'VUNJA BEI' 'ATUA POLISI'...AITAJA YANGA...