Home Habari za michezo AHMED ALLY: KIBU DENIS HAPASWI KUPEWA PRESHA…AKIPATIA ATAPATIA, AKIKOSEA ATAKOSEA TENA…

AHMED ALLY: KIBU DENIS HAPASWI KUPEWA PRESHA…AKIPATIA ATAPATIA, AKIKOSEA ATAKOSEA TENA…

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amejitokeza hadharani na kumkingia kifua Kiungo Mshambuliaji wa Klabu hiyo Kibu Denis.

Kiungo huyo amekuwa na wakati mgumu msimu huu, huku akionyesha kushindwa kuwajibika kwa kuifungia Simba SC mabao muhimu licha ya nafasi anazopata kila anapopewa nafasi na Kaimu Kocha Mkuu Juma Ramadhan Mgunda.

Ahmed Ally amechukua jukumu hilo, kwa kuandika ujumbe mzito kwenye kurasa zake za Mitandao ya Kijamii kuhusu Kibu, ambaye alisajiliwa Klabuni hapo mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Mbeya City FC.

Ahmed Ally ameandika: Kila mmoja hupitia nyakati ngumu kazini.

Kibu Denis anapitia nyakati hizo, jukumu letu ni kusimama nae na kumtia moyo ili isimuathiri, Kwenye football ukipatia utapatia tena, na ukikosea unaweza kukosea tena ni jukumu letu kumpa support ili asikosee tena.

Hatupaswi kumpa presha tunapaswa kumpa imani kwamba anaweza kufanya makubwa kama alivyofanya msimu uliopita

SOMA NA HII  KLABU YA SINGIDA FOUNTAIN GATE IMEELEZA MALENGO YAKE, HUKU AKILI YOTE IPO KWA SIMBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here