Home Habari za michezo BAADA YA KUGUNDUA MAYELE ATAKUWEPO KESHO…WATUNISIA WAANZA MBAMBAMBA ZAO MAPEMA…KOCHA WAO ALIA…

BAADA YA KUGUNDUA MAYELE ATAKUWEPO KESHO…WATUNISIA WAANZA MBAMBAMBA ZAO MAPEMA…KOCHA WAO ALIA…

Habari za Yanga

Kocha Mkuu wa Club Africain, Bertrand Marchand amesema moja ya staa wa Yanga anayemuhofia katika mchezo wa kesho wa mchujo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ni Fiston Mayele.

Kwenye kikosi cha Yanga, Mayele ndiye kinara wa mabao kwenye Kombe la Afrika baada ya nyota huyo kutupia jumla ya mabao saba katika hatua zilizopita dhidi ya Zalan kutoka Sudan Kusini na Al Hilal ya Sudan.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Marchand amesema Mayele ni mchezaji mzuri ambaye anamfahamu kwa muda mrefu tangu akiitumikia AS Vita ya kwao DR Congo.

“Wakati nipo klabu nyingine kabla ya hii miaka miwili nyuma nilihitaji kumsajili kwa sababu alinivutia sana kutokana na aina ya uchezaji wake ila bahati mbaya sikufanikiwa kwa hilo.” alisema Marchand.

Marchand aliongeza mbali na Mayele ila pia anawafahamu Tuisila Kisinda na Jesus Moloko japo Yanga ina wachezaji wazuri kutoka mataifa mbalimbali hivyo ni lazima wajiandae vizuri kutokana na ugumu wenyewe wa mchezo.

SOMA NA HII  RAIS SAMIA ABARIKI TANZANIA KUOMBA KUANDAA AFCON 2027...AHAIDI UJENZI WA VIWANJA VIPYA VITATU...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here