Home Habari za michezo BAADA YA KUONA SIMBA KAMA WAMEMCHUNIA HIVI…ADEBAYOR AWAPIGIA MAGOTI WAMSAJILI…

BAADA YA KUONA SIMBA KAMA WAMEMCHUNIA HIVI…ADEBAYOR AWAPIGIA MAGOTI WAMSAJILI…

Mshambuliaji wa kimataifa wa Niger ambaye anakipiga katika Klabu ya RS Berane ya Morocco, Victorien Adebayor amefunguka kwa mara ya kwanza juu ya maisha yake ndani ya timu yake mpya huku akiweka wazi kuwa safari yake ya mpira haijaishia hapo na ipo siku anaweza kuondoka.

Adebayor pia ameweka wazi ishu yake ya kutakiwa na Simba kabla ya kutua RS Berkane huku akisema timu hiyo kama bado wanahitaji huduma yake wanaweza kufuata taratibu za kumpata kwani kila kitu kinawezekana.

Nyota huyo amewaita Simba mezani kwa ajili ya kumsajili kutokana na kukutana na wakati mgumu ndani ya Berkane ambayo inanolewa na kocha Abdelhak Benchikha huku pia ikiwa imeondoshwa katika michuano ya kimataifa.

Ikumbukwe kuwa msimu uliopita Adebayor ndiye aliyeibuka mfungaji bora wa Kombe la Shirikisho Afrika akifunga mabao sita ambayo yaliwashawishi Berkane kumng’oa kutoka USGN ya kwao Niger.

Moja kwa moja kutoka Morocco, Adebayor alisema kuwa: “Kwa sasa mimi ni mchezaji wa RS Berkane lakini siwezi kusema kuwa nitaishi milele kama mchezaji wa hapa, maisha ya mpira ndivyo yalivyo leo naweza kuwa hapa kesho nikawa nipo sehemu nyingine.

“Kuhusu Simba unajua ni timu nyingine na mimi ni mchezaji wa timu nyingine hivyo sio sahihi kuwazungumzia wao, lakini kabla ya mimi kuwa hapa ni kweli walinihitaji lakini bado wanayo nafasi ya kufanya hivyo na wanafahamu nini cha kufanya kulingana na utaratibu ulivyo,” alisema winga huyo.

SOMA NA HII  WAKATI UONGOZI SIMBA WAKITAKA KOCHA MUAFRIKA...KOCHA WA AL AHLY AWAPIGIA SIMU NA KUWAPA NENO...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here