Home Habari za michezo BAADA YA MASHABIKI WA SIMBA KULIA KWAMBA ‘WANAOUMIA NI WAO’…TRY AGAIN AIBUKA...

BAADA YA MASHABIKI WA SIMBA KULIA KWAMBA ‘WANAOUMIA NI WAO’…TRY AGAIN AIBUKA NA KUWAJIBU HIVI…..

Habari za Simba

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, Salim Abdallah ‘Try Again’ ametoa pole kwa Wanachama na Mashabiki wa Klabu hiyo, kufuatia matokeo ya sare ya 1-1 dhidi ya Mbeya City.

Simba SC ilipata matokeo hayo jana Jumatano (Novemba 23) ikicheza ugenini Jijini Mbeya katika Uwanja wa Kumbukumbu ya sokoine, ikitangulia kufunga kwa bao la Mzamiru Yassin Kipindi cha Kwanza, lakini Mbeya City ilisawazisha kupitia kwa Tariq Seif Kiakala Kipindi cha Pili.

‘Try Again’ amewasilisha salamu hizo za pole kupitia Akaunti yake ya Mtandao wa Instagram akiandika: “Poleni Wanasimba wote. Tuna kazi ya kufanya mbele yetu.”

Simba SC imepoteza mchezo mmoja moja dhidi ya Azam FC (1-0), huku ikiambulia sare nne dhidi ya Young Africans, KMC FC, Singida Big Stars na Mbeya City.

Kwa mazingira hayo Simba SC inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 28, ikitanguliwa na Azam FC yenye alama 29 sawa na Young Africans iliyo kileleni.

Hali si shwari KMC FC, Majeruhi waongezekaYoung Africans bado ina michezo miwili mkononi, ikitarajiwa kushuka Dimbani Jumamosi (Novemba 26) kucheza dhidi ya Mbeya City katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

SOMA NA HII  EXCLUSIVE: MOHAMED HUSSEIN MKATABA WAKE UNAISHA SIMBA,

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here