Home Habari za michezo BENZEMA: RONALDO ‘KANILIA BUYU’ TOKA NISHINDE TUZO YA BALLON d’Or …

BENZEMA: RONALDO ‘KANILIA BUYU’ TOKA NISHINDE TUZO YA BALLON d’Or …

Mshambuliaji wa Real Madri, Karim Benzema amekiri kuwa mchezaji mwenzake wa zamani kikosini hapo, Cristiano Ronaldo hajampongeza kwa kushinda Tuzo ya Ballon d’Or aliyonyakua Oktoba mwaka huu licha ya urafiki mkubwa walio nao.

Ronaldo raia wa Ureno ambaye kwa sasa anaitumikia Man United, ameshashinda mataji mengi ikiwemo Ballon d’Or tano ambapo Benzema alishinda Tuzo hiyo hivi karinbuni katika ardhi ya nyumbani kwao, Lyon nchini Ufaransa.

Benzema amesema kuwa yeye ni miongoni mwa wachezaji waliofanya kazi kubwa kumsaidia Ronaldo kushinda kiatu hicho cha Dhahabu wakati wakishirikiana kucheza pamoja hasa mwaka 2018.

“Siku zote ninaamini katika mimi, nilijua kuwa kutokana na uwezo wangu na ndoto zangu pamoja na kujituma kwangu, ipo siku nitashinda tuzo hiyo. Ndiyo maana miaka nilipambana sana mpaka kupata tuzo hii,” Benzema aliiambia Téléfoot.

Alipoulizwa kuhusurafiki yake Ronaldo iwapo alimpongeza, Benzema alijibu “hapana, hajanipongeza”, licha ya tuzo hiyo kutolewa mapema mwezi uliopita.

Benzema ni Mfaransa wa kwanza kushinda tuzo hiyo tangu afanye hivyo Zinedine Zidane mwaka1998.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 34 amesema hana presha kuhusu timu yake ya Taifa ya Ufaransa kwenye Kombe la Dunia na ana amini watafanya vizuri huko Qatar na iwapo watachukua kombe hilo watakuwa wameshinda kwa mara ya tatu.

“Nina furaha sana kucheza Kombe hili la Dunia, nasubiri tu michuano ianze, nafahamu michuano hii ukubwa wake na umhimu wake, sina stress, natamani ianze mapema, tuonyeshe tuliocho nacho mbele ya mamilioni ya watu tukiliwakilisha taifa letu,” amesema Benzema.

SOMA NA HII  ZAKA ZAKAZI:- JUA KUWA KALI CHANZO CHA AZAM FC KUYUMBA....