Home Habari za michezo DODOMA JIJI HALI SI HALI….MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU…’WAFINYWA KISELA’ NA NAMUNGO

DODOMA JIJI HALI SI HALI….MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU…’WAFINYWA KISELA’ NA NAMUNGO

Dodoma Jiji imeendelea kujiweka pabaya baada kufungwa bao 1-0 dhidi ya Namung, mchezo wa Ligi Kuun uliochezwa uwanja wa Liti, Singida.

Dodoma katika penalti tatu ambazo imezipata katika michezo 13ilizocheza mpaka sasa imepoteza mbili na kupata moja.

Ushindi wa Namungo unakuwa wa tano katika msimu huu na kunaifanya timu hiyo kufikisha pointi 18 na kuendelea kubaki katika nafasi ya 8.

Dodoma Jiji inashika nafasi ya tatu kwa kufungwa mabao mengi yakiwa 18, huku kinara akiwa Mtibwa Sugar waliofungwa mabao 22 wakifuatiwa na Polisi Tanzania 19.

Namungo msimu huu na imefunga mabao 11 huku ikifungwa 11.

Bao la Abdulrazak Hamza linakuwa la 11 kwa Namungo huku mabao 6 yakiwa yamefungwa na mshambuliaji Reliant Lusajo.

Dodoma Jiji inaendelea kubaki na pointi 9 ikishika nafasi ya 15 kati ya timu 16 huku ikiwa imeshinda michezo miwili na kupoteza 8.

Katika mchezo wa leo mwamuzi Jackson Pallangyo kutoka Arusha alitoa kadi za nyano wachezaji wa Dodoma Jiji Hassan Kessy na Amani Kyata na kwa upande wa Namungo Frank Magingi na Hamis Swalehe.

SOMA NA HII  KISA KIPIGO KUTOKA KWA WAMOROCCO...MO DEWJI AIBUKA NA 'KAULI HII YA KIBABE' SIMBA...