Home Habari za michezo HUU NDIO UKWELI ULIVYO ‘BANA’….ACHA SIMBA WAJIFIE NA CHAMA WAO…

HUU NDIO UKWELI ULIVYO ‘BANA’….ACHA SIMBA WAJIFIE NA CHAMA WAO…

Chama na Simba SC Msimu Huu

Acha Klabu ya Simba wajivunie Chama wao! Wana haki na si jambo la ajabu timu kuwa na shujaaa wao.

Kwa miaka mingi FC Barcelona ilitengenezwa kumzunguka Lionel Messi kama ilivyo kwa Real Madrid na Cristiano Ronaldo (CR7).

Ukipiga kura za maoni pale jangwani kati ya Aziz Ki na Feisal nani auzwe, Aziz Ki ataoneshwa mlango wa kutokea licha ya mapenzi makubwa waliyonayo kwakuwa wanaijua thamani ya Feisal na mchango wake katika timu hiyo ya wananchi.

Simba ina wachezaji wengi wazuri lakini ukiutaka bora wa Simba SC kama timu lazima Chama awepo kwakuwa ndio muhimili wa timu katika kujilinda na kushambulia.

Ukongwe kwenye kikosi, exposure yake na kipaji vinamfanya awe hivyo na si jambo la ajabu kabisa kwa wanamsimbazi kuililia huduma ya mchezaji wao.

Kila zama zina mfalme wake katika timu na soka kwa ujumla ndio maana Bernado Silva kiungo mshambuliaji wa Manchester City amesema anaenda Qatar kuhakikisha Cristiano Ronaldo anabeba Kombe la Dunia zikiwa fainali zake za mwisho kabla ya kutundika daruga zake.

Silva licha yakuwa timu moja na CR7 lakini anatambua ufalme wa nahodha wake na kuupa priority. Denis Nkane pale Yanga SC amewahi kusema kuna siku atakuja waambia wanae alicheza timu moja na babu kaju ‘Sure Boy’.

“Binafsi huwa najiona mwenye bahati kubwa na Sure boy timu moja”. Hivyo mchezaji kukubalika na kubeba matumaini ya timu si ajabu na si kwamba anageuka kuwa mkubwa kuliko timu.

Wafalme katika timu wapo na wataendelea kuja mbaya tu ni wao kutumia ubora wao kusumbua viongozi. Wasenegali waliwagomea Bayern kuamini Sadio Mane hawezi kucheza kombe la dunia mwaka huu baada ya kuumia.

Wakatumia kila njia za kisayansi na kiasili lakini mwisho wa siku wamenyoosha mikono juu kwa uchungu. Hii yote ni kwa sababu wanaujua ubora na umuhimu wa mchezaji huyo katika timu na ushawishi nje ya uwanja.

Wachezaji kama Chama huongeza ari na moyo wa kupambana kwa wenzao pia hofu kwa wapinzani kwakujua muhimili upo ambao kocha anaweza kuupa majukumu kimbinu au deception plan kwa wengi.

SOMA NA HII  AHMED ALLY:- KIKOSI CHA PILI CHA SIMBA KWA MTIBWA NDIO KIKOSI CHAO CHA KWANZA....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here