Home Habari za michezo ISHU YA AUCHO YANGA BADO NJIA PANDA…NABI AVUNJA UKIMYA KINACHOENDELEA…

ISHU YA AUCHO YANGA BADO NJIA PANDA…NABI AVUNJA UKIMYA KINACHOENDELEA…

Habari za Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasredinne Nabi amewatoa hofu mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kutokuwa na wasiwasi kwa kukosekana baadhi ya wachezaji akiwamo Aziz Ki huku akitamba kuwa timu hiyo itacheza kikubwa kesho dhidi ya Kagera Sugar na kuwapa furaha.

Mbali na Aziz Ki ambaye amepewa ruhusa ya kwenda kwao nchini Burkina Faso, Nabi amesema bado hatma ya kiungo wao mkabaji, Khalid Aucho haijajulikana kama atakuwepo kesho baada ya kupata majeraha mchezo uliopita dhidi ya Club Africain lakini watamtazama kwenye mazoezi ya mwisho leo jioni na kupata ripoti ya madaktari ili kufahamu kama atatumika.

Nabi amesema licha ya mchoko walionao wachezaji, kukosa muda wa kujiandaa lakini timu hiyo itacheza kikubwa kesho na benchi la ufundi litakuja na mpango kabambe wa kupumzisha wachezaji bila kuathiri kiwango na ubora wa timu.

“Tangu tumecheza mechi ya Jumatano hatujafanya mazoezi kwahiyo tuta-train leo jioni kupitia hapo ndipo tutaona wachezaji gani tuwatumie, tutakuja na mpango ambao hata tukipumzisha wachezaji basi tuache balansi ya timu na kupata matokeo, hivyo tutawahamasisha wachezaji licha ya uchovu walionao kwa sababu hii ndiyo maana ya kujitoa mhanga,”

“Ni kweli tutamkosa Aziz Ki Yanga ni klabu kubwa haitegemei mchezaji mmoja tunatengeneza timu ambayo kila mchezaji anatimiza wajibu na kusaidia kupatikana kwa matokeo. Tunaamini falsafa tunayotumia ni kucheza hata mchezaji mmoja anapokosekana isipatikane hasara yoyote,” amesema Nabi.

Akizungumzia ubutu wa safu ya ushambuliaji katika michezo ya hivi karibuni amesema “Inafikia wakati wachezaji wanapitia kipindi cha mpito lakini tunafanya jitihada za kuhakikisha tunarejesha ubora wetu, tunaamini tunakwenda kucheza na timu ngumu ambayo imejiandaa na mwalimu mzuri,”

Mchezaji wa timu hiyo, Yusuph Athumani amewaahidi mashabiki wa Yanga ushindi kesho na kuwataka waje kwa wingi huku akitamba kuwa wachezaji wako imara kiakili na wanatambua majukumu yaliyowaleta jijini Mwanza.

“Tunaamini tunaweza kufanikisha kilichotuleta hapa kiakili tuko tayari na viongozi wetu wanatuamini, kitu kikubwa tunachoweza kuahidi ni ushindi kwa mashabiki wetu,” amesema Athuman.

SOMA NA HII  RASMI....MASOUD DJUMA KURUDI TENA BONGO...ISHU NZIMA IKO HIVI....