Home Habari za michezo KIPYENGA KIMELIA SIMBA….MABOSI WAPYA KUPATIKANA MWAKANI…RATIBA KAMILI IKO HIVI…

KIPYENGA KIMELIA SIMBA….MABOSI WAPYA KUPATIKANA MWAKANI…RATIBA KAMILI IKO HIVI…

Kamati ya Uchaguzi wa Klabu ya Simba imetangaza rasmi kufanyika uchaguzi wake mkuu Januari 29 mwakani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa klabu hiyo, Boniface Lihamwike amesema maamuzi hayo yamefikiwa baada ya viongozi walioko madarakani kumaliza muda wao.

“Simba inaenda kufanya uchaguzi wake mkuu ila nitoe tu angalizo kwamba kwa viongozi waliomaliza muda wao wataendelea kawaida na majukumu yao hadi tarehe ya uchaguzi,” amesema.

Lihamwike alisema katika uchaguzi huo nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti ambayo ni nafasi moja na wajumbe wengine wanne.

“Katika hao wajumbe wanne angalau mmoja awe Mwanamke pia kwa nafasi ya Mwenyekiti atakayechaguliwa katiba inamruhusu kuteua wajumbe wawili.”

Akitaja sifa zinazohitajika kwa wagombea, Lihamwike amesema mgombea yoyote yule anapaswa awe mwadilifu, Mwanachama hai wa Klabu na asipatikane pia na kosa la jinai.

Sifa nyingine ni umri kuanzia miaka 25 na asizidi 64, asiwe mwanahisa wa Klabu nyingine na asiwe Mwamuzi wa Mpira wa Miguu.

Kwa upande wa Mjumbe wa Kamati hiyo, Gerald Mongela amesema Disemba 5-19, itakuwa siku ya utoaji na kurudisha fomu za uchaguzi kwenye ofisi za Klabu ya Simba wakati Disemba 20-21, ni siku ya ukaguzi wa fomu zilizorudishwa ndani ya muda.

Disemba 22-24 ni tarehe ya usaili wa watia nia waliorudisha fomu ndani ya muda huku Disemba 28 itakuwa siku ya kubandika majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali ambao wamepita kwenye usaili.

Disemba 29-30 ni siku mapingamizi yote dhidi ya waombea huku Januari 1-2 mwakani itakuwa tarehe ya kupitia mapingamizi na kutoa wito kwa walioweka mapingamizi na wagombea waliowekewa.

Januari 3-4 ni siku ya kusikiliza mapingamizi na kutoa uamuzi huku Januari 5 itatumika kutangaza majina yote ya wagombea waliokidhi vigezo.

Kuanzia Januari 6-28 itakuwa ni tarehe rasmi za kuanza kampeni kwa wagombea na ikifika Januari 29 itakuwa siku muhimu ya uchaguzi mkuu.

SOMA NA HII  SIMBA SC TABU IKO PALEPLE.....HIZI HAPA SIKU 61 ZA JASHO, MACHOZI YA DAMU..WAKIZINGUA IMEKULA KWAO....