Home Habari za michezo KISA ‘KUILOGA’ SIMBA…TFF WAISHUSHIA RUNGU LA ADHABU SINGIDA BIG STARS…

KISA ‘KUILOGA’ SIMBA…TFF WAISHUSHIA RUNGU LA ADHABU SINGIDA BIG STARS…

Singida Big Stars

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi ya Bodi ya ligi kuu Tanzania (TPLB) imemfungia mechi tatu (3) na faini ya Tsh 500,000 beki wa Klabu ya Singida Big Stars Shafiq Batambuze kwa kosa la kuingia uwanjani kupasha misuli moto kabla ya muda ulioruhusiwa.

Batambuze aliingia dakika 10 kabla kwenye mchezo dhidi ya Simba ulioisha kwa sare ya mabao 1-1 na alionekana akimwaga vitu kama maji uwanjani vitendo vilivyoashiria kuwa ni imani za kishirikina.

Maafisa wa TFF walimtaka arudi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo hata hivyo Kocha Msaidizi wa Singida Big Stars Mathias Lule na Kocha wa magolikipa Steven Kiagundu walimuamuru aendelee kubaki uwanjani licha ya Batambuze kuanza kutoka uwanjani.

Makocha hao wamefungiwa mechi 3 na faini ya Tsh 1,000,000 kila mmoja kwa makosa hayo.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA WACHEZAJI WAKE 'WAKIRUKA RUKA' JUZI MBELE YA WAARABU...ZORAN AVUNJA UKIMYA SIMBA...ATAKA STRAIKA..