Home Habari za michezo KISA SIMBA NA YANGA…WADHAMINI LIGI KUU WAIBUKA NA HOJA MPYA…WAWEKA WAZI VIAUMBELE...

KISA SIMBA NA YANGA…WADHAMINI LIGI KUU WAIBUKA NA HOJA MPYA…WAWEKA WAZI VIAUMBELE VYAO…

Ligi Kuu Tanzania 2023/24

Mkurugenzi wa fedha na utawala wa NBC ambao ni wadhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Waziri Barnabas amesema imefika wakati wa kuifanya dabi ya Kariakoo kuwa na thamani zaidi ya kutazama tu dakika 90.

Amesema dabi ya Kariakoo inavutia maelfu ya mashabiki duniani hivyo haipaswi kuishia ndani ya dakika 90 za uwanjani bali Shirikisho (TFF) na klabu husika zitengeneze utaratibu ambao wageni wanaokuja kutazama dabi hiyo watafurahia ikiwamo kutembelea vivutio vya utalii.

Amesema mbali na mchezo huo dabi nyingine ndani ya Ligi Kuu ikiwamo Mzizima na Mbeya derby zinapaswa kupewa thamani ili kuongeza ushindani na mvuto kwenye mashindano hayo.

“Tuzipe hadhi dabi zetu kuongeza watazamaji kuanzia Kariakoo, Mzizima na Mbeya tuongeze ushindani,”

“Soweto debry ni kubwa sana watu hawaendi tu kutazama mpira bali kufanya utalii, tufanye hivyo tuitumie dabi kwa mambo chanya na kuvutia watu wengi watamani kuja kwenye mechi hii,” amesema Barnabas.

Amesema wameandaa utaratibu wa kutoa mabasi kwa timu za Ligi Kuu kwa mkopo ambapo ameziomba kuandaa maandiko ambayo yatawezesha kupatikana mabasi hayo kwani kwa sasa wameanza na Coastal Union na Shirikisho la Soka.

“Tunajivunia kwamba sisi ni sehemu ya mafanikio ya soka la Tanzania na bado tupo sana, tumekuwa benki ya kwanza kutoa bima kwa wachezaji, benchi la ufundi na familia zao,” amesema.

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia akizungumzia thamani ya Dabi amesema amepokea ushauri huo ambao wataufanyia kazi huku akiwashukuru kwa kuendelea kuunga mkono maendeleo ya soka nchini

SOMA NA HII  MWAMBA KAGOMA KUSEPA NANI ATOKE SIMBA !?