Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA POLISI TZ LEO…SIMBA WAWEKA MATUMAINI KWA WAZAMBIA WAKE…

KUELEKEA MECHI NA POLISI TZ LEO…SIMBA WAWEKA MATUMAINI KWA WAZAMBIA WAKE…

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda, ni kama amewakabidhi viungo washambuliaji wa timu hiyo, Clatous Chama na Moses Phiri kuhakikisha wanatengeneza nafasi nyingi za kufunga na kuzitumia ipasavyo ili kupata matokeo mazuri.

Simba leo Jumapili, wapo ugenini kwenye Uwanja wa Ushirika, Moshi mkoani Kilimanjaro kucheza dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Kocha Mgunda alisema kikosi chake ni kweli kimekuwa kikitengeneza nafasi, lakini ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri dhidi ya Polisi Tanzania, basi wanatakiwa kutengeneza nafasi nyingi zaidi ya kawaida na kuzitumia ipasavyo.

“Ni kweli timu imekuwa inatengeneza nafasi, lakini zimekuwa siyo nyingi na kuanzia katika uwanja wa mazoezi tumekuwa tukifanyia kazi jambo hilo na kwa sasa imebaki kwenda kwa wachezaji wetu kufanya uwanjani.

“Tunatakiwa kuhakikisha tunatengeneza nafasi nyingi za kutosha ili washambuliaji wapate nafasi za kufunga na itakuwa salama kwetu kupata matokeo mazuri zaidi, ushindi kwetu ndio jambo la msingi katika michezo iliyosalia kuanzia huu,” alisema kocha huyo.

Msimu huu, Simba imekuwa na mwendo wa kusuasua katika Ligi Kuu Bara ambapo inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 28 baada ya kucheza mechi 13.

SOMA NA HII  KUHUSU PABLO KUFUKUZWA ...MECKY MEXIME AWALIPUA MABOSI SIMBA...ADAI WAMEKURUPUKA KABLA YA KUFIKIRI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here