Home Habari za michezo MGUNDA NAYE ASHINDWA KUJIZUIA KUHUSU KIBU DENIS…AFUNGUKA KUHUSU WAKATI WAKE…

MGUNDA NAYE ASHINDWA KUJIZUIA KUHUSU KIBU DENIS…AFUNGUKA KUHUSU WAKATI WAKE…

Habari za Simba

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wakati wa kufunga kwa mshambuliaji wake Kibu Dennis unakuja.

Nyota huyo msimu wa 2021/22 alikuwa mfungaji bora ndani ya kikosi cha Simba alipotupia mabao 8 kibindoni.

Msimu huu hajafunga bao zaidi ya kutoa pasi moja ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons alipompa mshikaji wake Jonas Mkude.

Mgunda amesema:”Kwa sasa kila mchezaji anatimiza majukumu yake ndani ya timu na nina amini kwamba kwenye upande wa ufungaji tutakuwa vizuri pia.

“Kuhusu Kibu mwanangu wakati wake unakuja na atafunga hivyo ni suala la kusubiri kila kitu kitakuwa sawa,” amesema.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO.....AHMED ALLY AFUNGUKA ISHU YA JOHN BOCCO NA HOFU ILIYOKUWEPO...ATOA OMBI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here